Mkuu wa mkoa wa Arusha ametembelea eneo linalojengwa hospitali ya wilaya ya Karatu, ziara hiyo ililenga kujionea maendeleo ya ujenzi wa hospitali ya wilaya pamoja na kupata taarifa ya ujenzi wa hospitali.
Ujenzi wa hospitali ya wilaya ya karatu ulianza baada ya wilaya kupokea kiasi cha shilingi 500,000,000.00 kutoka mamlaka ya hifadhi ya Ngorongo. Halmashauri ilitenga kiasi cha shilingi 32, 000, 0000.00 kwa mwaka wa fedha 2018/2019. Mpaka sasa mradi una majengo matatu , jengo la utawala na jengo la maabara yapo katika hatua ya lenta na jengo la wagonjwa wa nje limeshaezekwa majengo. Mhe Mrisho Gambo amesema kuna kulegalega kwenye usimamizi wa ujenzi wa hospitali ya wilaya. Ametoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa wilaya ya Karatu kuongeza usimamizi katika ujenzi wa hospitali. Mhe. Gambo amesema Mamlaka ya hifadhi ya ngorongoro imeahidi kutoa million 100 kwa mwaka huu wa fedha kukamilisha jengo la maabara na jengo wagonjwa wa nje.
Ameongeza kusema Serikali pia imetoa milioni 500 nyingine kwa mwaka huu wa fedha kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya wilaya, fedha ambazo zinatarajiwa kutumika kuongeza idadi ya majengo katika ya hopitali ya wilaya. Wizara ya tawala za mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI ilichelewa kupata taarifa za maendeleo ya ujenzi wa hospitali ya wilaya. Amesema fedha zilizotolewa na wizara ni kwa ajili ya ujenzi wa jengo la utawala jengo la wagonjwa wa nje na jengo la maabara na tayari ujenzi ulishafanyika na umefikia katika hatua mbalimbali. Ametoa maelekezo kwa Mkuu wa wilaya na Mkurugenzi wa Halmashauri kuandika barua ya clarification kwa wizara ya tawala za mikoa na serikali za mitaa juu ya ujenzi wa majengo hayo matatu ambayo yameshajengwa. Ili million 500 za serikali zilizotolewa zijenge majengo mengine badala ya hayo matatu, amesema hospitali ya wilaya inapaswa kuwa na majengo saba.
Naye Mkuu wa wilaya ya Karatu Mhe.Theresia Mahongo amesema atafuatilia kuhakikisha ujenzi wa hospitali ya wilaya unakamilika kwa wakati. Amesema atatumia wahandisi wa ujenzi wa Tarura ili kupata ushauri wa kitaalamu hasa katika ujenzi wa majengo hayo mapya yanayotarajiwa kujengwa. Mhe. Mahongo amesema wananchi watajitolea nguvu kazi ya kujenga msingi kwa majengo hayo mapya yanayotarajiwa kujengwa. Ameomba serikali kuharakikisha kutoa million 500 ili waweze kuhakikisha ndani miezi mitatu ujenzi wa majengo uwe umekamilika. Mhe. Mahongo ametoa salamu za shukurani kwa niaba ya wananchi wa wilaya ya Karatu kwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa fedha zilizotolewa kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya wilaya.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Karatu Mhe Emmanuel Gege amesema swala la ujenzi wa Hospitali ya wilaya litakuwa ajenda kuu kwa sasa. Amesema yeye kama muwakilishi wa wananchi atashirikiana na watendaji kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati. amesema watatumia pia mawazo mbadala kuhakikisha ujenzi unaenda haraka, Mhe. Gege ameshukuru viongozi kwa kulisimamia kidete swala la ujenzi wa hospitali ya wilaya.
Picha ni Muonekano wa nje wa jengo la wagonjwa wa nje baada ya kuezekwa
Mkurugenzi Mtendaji ndugu Waziri Mourice amesema watendaji wa Halmashauri wamefikiria kutumia fedha za ndani million 40 kukamilisha majengo mawili ya maabara na jengo la wagonjwa wa ndani. Amesema watendaji watatumia uadilifu kukamilisha mradi wa ujenzi na kuhakikisha wanasimamia vizuri matumizi ya fedha za ujenzi wa majengo hayo mawili ili yaanze kutumika ifikapo mwezi wa saba mwaka huu.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa