Na Tegemeo Kastus
Kasi ya usambazaji wa umeme wa REA vijijini kupitia mkandarasi NIPO bado ni ndogo katika wilaya ya Karatu. Mhe Gambo amesema ataenda kwenye Yard ya Kampuni hiyo ili kukagua idadi ya transfoma, nguzo na nyaya za kusambaza zilizopo katika ofisi kuu iliyopo Arusha.
Mh. Gambo amesema hayo wakati alipofanya ziara Kijiji cha Endala kukagua kazi ya usambazaji wa umeme wa REA. Mh. Gambo amewaambia wananchi kwamba nguzo haziuzwi, nguzo ni mali ya serikali amesema mwananchi yeyote asiuziwe nguzo kwa ajili ya umeme wa REA. Gharama za usambazaji wa umeme ni shilingi 27000.
Mkandarasi amebakisha miezi miwili kukamilisha usambazaji, amesema Uongozi wa mkoa mwezi wa nane umejianda kupokea miradi yote ya umeme. Mh. Gambo amesema mkandarasi NIPO ni kampuni ya wazawa lazima wafanye kazi vizuri kuonesha kwamba wakandarasi wazawa wanafanya kazi vizuri.
Mh. Gambo amempongeza mkuu wa wilaya ya Karatu kwa jitihada zake za kufuatilia na kuweka mkazo katika usambazaji wa umeme vijijini. Mh. Gambo ametoa maelekezo kuweka umeme katika eneo la kisima cha usambazaji wa maji ili kupunguza gaharama za huduma ya maji na kusambaza umeme katika tasisisi za umma kama Hospitali na Shule.
Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Theresia Mahongo amesema nguzo zimewekwa mda mrefu lakini nyaya hazijaunganishwa. Amesema amefuatilia kwa karibu sana zoezi la usambazaji wa umeme katika kijiji cha Endala amesema eneo hilo lipo karibu na ziwa Manyara. Amesema umeme ukiwekwa katika kijiji hicho mwanga wa taa utasaidia wanyama wakali kuondoka eneoa hilo ambalo limepakana na hifadhi ya ziwa manyara.
Akieleza matarajio yake Mwenyekiti wa kijiji Thomas Essau amesema amefurahia ujio wa mkuu wa mkoa wa Arusha, amesema wamefarijika kuona barabara imetengenezwa vizuri. Amesema ziara hiyo itasaidia kujua hatima yao ya kupata umeme wa REA.
Muwakilishi wa kampuni ya NIPO Ndg. Goima Msimbira amesema changamoto ya kazi wanayofanya ni uhaba wa nyaya ili wasambaze umeme kwa vijiji. Amesema wameshakaa vikao na muajiri wao REA na (Supplier) wakala wa usambazaji wa vifaa pamoja na NIPO. Kikao walichokaa pamoja kulijadili namna gani watapata vifaa kwa wakati ili kazi iendelee amesema nguzo kukaa eneo la kazi mwaka mzima si jambo la kawaida.
Amesema makubaliano waliofikia pamoja na mpango wa kazi wao na namna mleta vifaa (supplier) atakavyoleta vifaa kwa wakati ameahidi kwa wananchi mpaka june 30 mwezi huu 2020 umeme utakuwa tayari umeshasambazwa. Amesema nyaya zimeshafika katika ofisi zao kuu Arusha na wataanza kazi ya kuzisambaza.
Naye Mwanchi Maria Yakobo amesema mara baada ya nguzo kuwekwa walipata matumaini lakini matumaini yao yakafifia kwa sababu mradi umekaa muda mrefu bila kujua kinachoendelea . Lakini kutokana na ziara hiyo ya mkuu wa Mkoa imeleta Tumaini jipya kwamba kijiji cha Endala kimewekwa katika kipaombele cha kupatiwa huduma za umeme mapema.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa