NA TEGEMEO KASTUS
Wilaya zote zitakuwa na mabaraza ya wazee mpaka kufika mwezi wa kumi na moja mwishoni.Wilaya ambazo mpaka sasa hazina baraza la wazee ni Karatu, Ngorongoro na Longido, baada kuunda mabaraza utaratibu utawekwa kuhakikisha wazee wanashiriki katika vikao vya ngazi zote kuanzia kata mpaka wilaya.
Hayo yamesemwa na Mh. Iddi Kimanta Mkuu wa Mkoa wa Arusha wakati akizungumza katika sherehe ya siku za wazee yaliyofanyika wilaya ya karatu kimkoa, yenye kauli mbiu familia na jamii tuwajibike kuwatunza wazee. Mh. Kimanta ameahidi kuwezesha mkutano wa baraza la wazee la Mkoa amesema mkoa utatoa usafiri kwa viongozi wa Mkoa kutembelea mabaraza ya wazee ya wilaya ili wahamasishe kuunda Mabaraza ya viongozi.
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mh. Iddi Kimanta (kulia) akipokea maandamano katika maadhimisho ya siku ya wazee yaliyofanyika katika uwanja wa mazangira bora Karatu
Mh. Kimanta amesema kwa kushirikiana na viongozi wa Mkoa na wilaya katika kusimamia maswala yote yanayohusu wazee, kwa matendo yanayostahili kuwapatia heshima. Ameomba wazee kuwa na imani na serikali, amesema maendeleo yanayofanywa na serikali kila mtu anamchango wake.
Mh. Kimanta amesema mtu yeyote anayebeza wazee hajui anaelekea wapi, Amesema kwa kushirikiana na viongozi wa mkoa na wilaya huduma za afya kwa wazee zitaimarishwa, ikiwa na pamoja vitambulisho vya wazee.
Awali katika risala ya wazee iliyosomwa na Mzee Hamisi Ramadhani katibu wa baraza la wazee mkoa wa Arusha amesema dawa za kutibu wazee kwa maradhi yasiyoambukizwa zimekuwa duni na dawa hizo ni gharama kuzipata. Amesema wazee wengi wanaishi katika mazingira magumu inayosababishwa na umaskini na kukosa lishe bora, makazi na huduma nyingine muhimu za kibinadamu kwa sababu ya hali hii baadhi yao imewasababisha wazee wengine kupata ulemavu ikiwa ni pamoja na miili yao kupooza.
Mzee Ramadhani amesema baadhi ya wilaya kama Meru-dc Arusha-mc, Arusha-dc zimeanza kuwashirikisha wawakilishi baraza la wazee kwenye vikao muhimu kama vya vikao vya maendeleo vya kata na Wilaya. Mzee Ramadhani ameomba wilaya ambazo haziajatekeleza zianze kufanya hivyo haraka. Amesema serikali bado haijatunga sheria ya wazee baada ya sera ya wazee iliyotoka takribani miaka 17, ameomba serikali kukamkamilisha kutunga sheria za wazee kulingana na mahitaji ya sasa.
Katika taarifa ya Mkoa iliyosomwa na Ndg. Denis Mgiye amesema katika jitihada za kutoa huduma kwa haraka kwenye vituo vya afya wameweka ujumbe unaosema “ kwanza mpishe mzee apate huduma.” Jumla ya mabaraza ya wazee 718 kati ya mabaraza 732 yanayopaswa kuundwa yameundwa katika ngazi ya kijiji mtaa mpaka mkoa. Amesema mkoa umetekeleza maelekezo ya kuwatambua wazee na mpaka sasa wazee 97497 wametambuliwa na wazee wamepatiwa vitambulisho 37262 ambayo ni sawa na 56%.Ndg. Mgiye amesema Halmashauri ya Meru-dc Arusha-dc Arusha mc na Monduli-dc zinaongoza kwa kuwapatia wazee vitambulisho.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa