Na Tegemeo Kastus
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mh. Mrisho Gambo ametoa siku 20 kwa uongozi wa kata ya Mbulumbulu kusimamia ujenzi wa jengo la mionzi (X-ray) katika kituo cha afya Kambi ya simba kuwa umemalizika.
Awali ujenzi wa jengo hilo ulisimama kusubiri ukaguzi wa wataalamu wa mionzi ili liweze kuendana na ubora pamoja na mahitaji. Wataalamu wa mionzi wameshakagua jengo hilo, na ujenzi wa jengo umeruhusiwa kuendelea kwa kufuata maelekezo ya wataalamu wa mionzi. Halmashauri ya wilaya ya Karatu ilichangia kiasi cha 5,000,000.00 kwa ujili ya ujenzi wa jengo hilo na Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro ilichangia kiasi cha 20,000,000.00 kusadia ujenzi wa jengo hilo kukamilika.
Mh. Gambo ameyasema hayo katika ziara ya siku moja alipotembelea Hospitali ya Wilaya, kituo cha afya Kambi ya simba na kituo cha afya Endabash. Mh. Gambo ameoneshwa kutoridhishwa baada ya kukuta baadhi ya vifaa vya kitaalamu ambavyo vimeletwa kutoka MSD muda mrefu lakini bado havijaanza kutumika. Ametoa maelekezo kwa wataalamu wa afya kuhakikisha vifaa hivyo vinaanza kutumika mapema iwezekanavyo. Mh. Gambo amesema (TAMISEMI) imetenga million 300 kwa ajili vifaa tiba ambavyo vimeagizwa MSD kwa ajili ya kituo cha afya Endabash. Amesema atawasiliana na watu wa MSD ili kuharakisha upatikanaji wa vifaa hivyo ili viweze kuanza kufanya kazi na kusaidia wananchi.
Mh. Gambo amewahimiza wananchi kujitolea katika ujenzi wa jengo la maabara katika Kituo cha afya Endabash, ambacho Halmashauri imekitengea shilingi million 40 kwa ajili ya ujenzi wa Maabara. Wananchi wa Endabash kupitia Mwenyekiti wa kijiji wamekubali kuchangia mchango wa shilingi 5000 kwa kila kaya, pamoja na kujitolea nguvu kazi ya kuchimba msingi, kuleta kokoto na ukusanyaji wa mawe. Mh. Gambo ameahidi kutoa mchango wa shilingi million moja kwa ajili ya ujenzi wa maabara katika kituo cha afya Endabash.
Mh. Mrisho Gambo (katikati) akiwa katika ukaguzi wa kituo cha afya Endabash
Mh. Gambo ametoa maelekezo kwa Maafisa Tarafa pamoja na watendaji wa chini yao katika maeneo yao ya uongozi kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko wa bima ya afya iliyoboreshwa (ICHF). Mfuko huo ni shilingi 30,000 kwa baba na mama na wategemezi wanne kwa mwaka, ili wananchi kukwepa gharama za kulipia fedha kila wanapoenda hospital kwa ajili ya matibabu.
Mh,Gambo ametembelea Mradi wa maji wa kwa Tom, wilayani Karatu, mradi unaozalisha lita 50,000 kwa saaa. Mh. Gambo amesema sekta ya maji ilikuwa na miradi iliyokuwa imekatiwa tamaa kwa sababu fedha zilikuwa zinatengwa lakini matokeo yalikuwa hayaendani na thamani. Amemshukuru Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli; amesema ameacha alama kubwa sana, na amewapaongeza mamlaka ya maji Auwsa kwa ujenzi wa miundo mbinu ya miradi huo wa maji uliogaharimu takriban million 600 mpaka kukamilika kwake. Mradi wa maji wa kwa-Tom umesaidia wananchi wa Karatu mjini kuepuka adha ya shida ya maji, amesema awali mradi wa maji uligharimu million 700 hivyo Auwsa imefanya kazi kwa fedha pungufu kulingana na kiwango kilichowekwa awali. Amesema Auwsa imekabidhiwa kazi nyingine visima vya Ayalabe na Bwawani, serikali ya awamu ya tano kwa kupitia wizara ya maji imeshavitengea million 200 kwa ajili ya kazi ya awali kwenye visima hivyo. amesema sasa ni lazima miradi hiyo ya maji itunzwe, ili miradi hiyo ya maji isihujumiwe.
Mh. Mrisho Gambo (katikati) akipata maelekezo kutoka kwa mwandisi Lunjomba kwenye moja ya tanki la maji lilopo wilayani Karatu
Mh. Theresia Mahongo Mkuu wa wilaya ya Karatu amemepongeza Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuleta fedha kwaa miradi ya maji Karatu. amepongeza Mwandishi wa maji Injinia Lunjomba kwa kusaidia upatikanaji wa maji safi kwa wakazi wa Karatu. Amesema isingekuwa mradi wa maji kwa-Tom wananchi wa Karatu wangepata shida kubwa ya maji kwa sababu kisima cha bwawani kimeshindwa kufanya kazi kutokana na mvua zinazoendelea kujaza maji katika eneo hilo na kuathiri mashine za maji zilizo katika eneo hilo.
Meneja wa maji wa Auwsa Mwandisi Lunjomba amesema mradi wa kwa-Tom umebakiza fedha kidogo kwenye bajeti takribani million 95. Amesema wanadhamiria kuziombea kibali fedha hizo kwa ajili ya kujenga miundo mbinu ya maji katika eneo linalojengwa hospitali ya wilaya ya Karatu.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa