NA TEGEMEO KASTUS
Miradi ya ujenzi iliyofanyika katika Halmashauri ya wilaya ya karatu, imesimamiwa na kujengwa kwa ubora unaotakiwa. Umakini huu wa ujenzi wa miradi ya maendeleo utaendelea kuwepo na tutaendelea kusukuma maendeleo ya mkoa wa Arusha. Lengo la serikali ni kuhakikisha huduma kwa wananchi zinapatikana kwa urahisi na kwa viwango vinavyotakiwa.
Hayo yamesema na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh. John Mongela katika ziara yake ya kwanza katika wilaya ya Karatu alipokuwa akitembelea miradi ya maendeleo itakayozinduliwa na kuwekewa jiwe la msingi na mwenge wa uhuru mapema mwezi june mwaka huu. Katika ziara hiyo Mkuu wa mkoa wa Arusha alitembelea jengo la maabara katika kituo cha afya cha Endabash, jengo ambalo mpaka sasa limegharimu kiasi cha million 23 katika ujenzi wake na likitarajiwa kumalizika tarehe mosi mwezi wa kumi.
Mh. Mongela amesema lazima majengo yafanye kazi, majengo yasipotumika yanaharibika na badala yake serikali inaanza kutoa fedha za ukarabati. Amesema jengo la maabara, jengo upasuaji na jengo la mama na mtoto na wodi ya watoto vilivyojenga katika kituo cha afya Endabash vitoea huduma ya afya kama inavyopaswa. Ili wananchi wapate huduma za msingi bila kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya. Amesema ujenzi wa jengo la maabara ukikamilika vipimo vyote vitakuwa vinapatikana katika kituo cha afya cha Endabash na huo ndio Mkakati wa serikali ya awamu ya sita.
Katika hatua nyingine Mh. Mongela ametembelea shule ya sekondari ya Florian amesema lazima sasa mkakati wa kufuta ufaulu wa daraja la nne kwa wanafunzi uanze. Ili ufaulu wa wanafunzi uwe daraja la kwanza daraja la pili na daraja la tatu. Mh. Mongela ametembelea mradi wa ujenzi wa madarasa matatu uliojengwa na fedha za mfuko wa EP4R na ameoneshwa kuridhishwa na ujenzi wa madarasa uliofanyika katika shule ya sekondari ya Florian.
Mh. Mongela akikagua miundo mbinu ya kituo cha afya Endabash
Awali katika kikao cha ndani Mh. John Mongela akizungumza na wakuu wa idara na vitengo taasisi na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama amesema lazima watendaji wa serikali watimize wajibu wao katika maeneo yao ya kazi. Lazima kila mtumishi katika eneo alipo athibitishe uwepo wake katika utendaji mzuri wa kazi.
Mh. Mongela amesema lazima kuwe na usimamizi mzuri katika ukusanyaji wa mapato lakini pia lazima kuwe na usimamizi na matumizi mazuri ya fedha zinatokana na makusanyo ya ndani. Ameongeza kusema lazima miradi ya maendeleo inayojengwa na inayotarajiwa kujengwa iwe na ubora inaotarajiwa. Amesema mambo hayo yakizingatiwa Halmashauri haiwezi kuwa na hoja za ukaguzi, amesema hatavumilia kuona jambo lolote linatoa watendaji katika utaratibu wa kufuata sheria katika utendaji wa kazi.
Mh. Mongela akitoa kukagua ujenzi wa vyumba madarasa katika shule ya sekondari Florian
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa