Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.Mrisho Gambo ameendelea na ziara yake wilayani Karatu kwa siku ya pili. Katika ziara yake ameweka jiwe msingi kwenye bweni la wasichana pamoja na nyumba mbili za walimu (two in one) shule ya sekondari Baray Khusumay katika kijiji cha Khusumay.
Mhe. Gambo ameipongeza TASAF kwa miradi yake ya awamu ya tatu, amesema majengo yamejengwa vizuri. Amewapongeza pia wananchi kwa kujitolea nguvu kazi zao katika ujenzi wa shule. Amesema mwaka huu madarasa mawili yatachukua wanafunzi na madarasa mawili yatatumiwa na walimu kama ofisi. Mwaka ujao wa fedha wanafunzi watatumia madarasa mawili yaliyobakia hivyo kuna umuhimu wa kuanza ujenzi wa jengo ya utawala mapema. Kila mtu lazima ashiriki shughuli za maendeleo katika eneo lake. Mkuu wa mkoa ametoa bati 100 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la utawala shule ya Baray Khusumay na mkuu wa wilaya ya Karatu ametoa shilingi 500000 na Mkurugenzi wa halmashauri ametoa mifuko 100 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa jengo hilo. Katika tukio hilo wananchi wamekubali kutoa shilingi 25000 kila kaya kwa ajili ya ujenzi wa jengo la utawala la shule ya Baray Khusumay. Wananchi wameridhia ifikapo mwisho wa mwezi wa sita kulipa kiasi hicho ili kuanzia mwezi wa saba ujenzi wa jengo la utawala uanze.
Mhe. Gambo amesema Mwaka 2018 mkoa ulikuwa na wanafunzi 18000 waliomaliza darasa la saba na kukosa maeneo ya kusoma. Amesema ilibidi maeneo mengine tuweke wanafunzi wengi kinyume na sera ya elimu. Lakini tukajiwekea mkakati wa kujenga nyumba za walimu, madarasa, kujenga mabweni ili tuwapunguze wanafunzi sehemu walizozidi wakae darasani kwa mujibu wa sera ya elimu. Mhe. Gambo amesema amefurahi kuona shuke imesajiliwa. Shule hiyo itapokea wanafunzi kuanzia mwezi wa saba walioenda shule za jirani.
Mratibu wa TASAF wilaya ya Karatu Bi, Restiel Hayuma amesema kijiji Khusumay kina kaya 430 na wakazi 2408. Amesema kijji kina kaya 83 ambazo zinanufaika na miradi ya TASAF, kijiji hiki ni miongoni mwa vijiji 39 vinavyonufaika na miradi ya TASAF. Miradi ya nyumba 2 za walimu na bweni la wanafunzi imejengwa na miradi ya Tasaf awamu ya tatu ambayo shilingi milion 320989495. Fedha zilizotolewa na mradi wa TASAF ni shilingi 271420595 na wananchi wametoa shilingi 49568900 kwa kufanya kazi wakati wa ujenzi, na kutoa vitendea kazi na vifaaa vya ujenzi kama mawe na kokoto.
Mkuu wa mkoa Mhe. Gambo akikagua nyumba za walimu shule ya Baray Khusumay.
Mkuu wa mkoa wa arusha Mhe. Gambo akikagua bweni la wasichana Baray Khusumay.
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Gambo akiondoa kitambaa katika bweni la Baray Khusumay kama ishara ya kuweka jiwe la msingi.
Mkuu wa Mkoa wa arusha Mhe.Gambo akiondoa kitambaa kwenye nyumba ya walimu two in one kama ishara ya kuweka jiwe la msingi.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa