Mkuu wa wilaya ya Karatu Mhe. Theresia Mahongo amezindua kampeni ya “jiongeze, tuwavushe salama tupunguze vifo vitokanavyo na uzazi. Uzinduzi huo umefanyika katika ukumbi wa Halimashuri ya wilaya ya Karatu na ulihudhuriwa na wadau mbalimbali wa afya.
Mhe. Theresia amewapongeza sana wafanyakazi wa sekta ya afya kwa kuendelea kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi. Ametoa wito kwa wakunga wa jadi kuendelea kushirikiana na watendaji wa afya wa serikali na kuendelea kuwahamasisha kina mama wajawazito kuhudhuria vituo vya afya. Amesema lengo letu ni kuhakikisha wakina mama wanajifungua salama na kupunguza vifo vinvyotokana na uzazi. Amesema serikali imeongeza fedha ktika idara ya fedha ili kinamama watarajiwa na watoto wa umri chini ya miaka mitano wapate huduma ya afya bure. Amewapongeza wadau wa afya wanaoshirikina na serikali, amesema kazi inaoenekana na natambua mchango wenu katika kuimarisha afya ya mama na mtoto. Amewaomba kuzidi kushiriki katika kuongeza rasilimali zote muhimu zitazolenga kuboresha afya ya mama na mtoto katika wilaya ya karatu.
Mhe. Theresia ametoa wito kwa Maafisa tarafa, kusimamia hatua zote muhimu ili kupunguza vifo vya uzazi na watoto wachanga. Amesema kila mtendaji afanye ajenda ya afya ya mama na mtoto kuwa ajenda muhimu katika vikao vyake. Amesema ni matumaini kwamba maafisa tarafa watafuatilia kwa umakini taarifa za afya kwa ngazi zote ndani ya tarafa ili taarifa za kinamaa wajawazito na watoto wachanga ziwekwe na kutunza vizuri. Maafisa tarafa wamesaini hati ya kiapo ya kutekeleza majukumu hayo mbele ya mkuu wa wilaya ya Karatu Mhe. Theresia Mahongo na kaimu mkurugenzi Mtendaji wa wilaya, ndugu Godfrey Luguma.
Amesema sababu nyingi za vifo vitokanavyo na uzazi pamoja na vifo vya watoto wachanga zinazuilika, ndio maaana tunahamasisha jamii itoe elimu ya afya ikiwa pamoja na kuhamasisha wananchi kupenda kuhudhuria kiliniki. Mhe. Theresia amesema kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi ni swala mtambuka amehimiza ushirikishawaji viongozi wa dini, viongozi wa vijiji vitongoji na madiwani ili kusaidia kuhamisha wakinamama wajawazito kupenda kuhudhuria hospitali.
Awali katika taarifa yake Mganga mkuu wa wilaya Dtk Musatafa Waziri amesema kuna ucheleweshaji wa mama mtarajiwa ngazi ya jamii. Amesema wakinamama wajawazito huwa wanajifungulia nyumbani hawafiki vituo vya kutolea huduma mapema. Amesema kuna swala la mila ambalo linafanya mama mtarajiwa kutokuwa na maamuzi ya kwenda hospitali, au kutumia dawa za kienyeji badala ya kufika hospital au kituo cha afya. Jambo linalosababisha mama kupata uchungu kabla ya muda; wakati mwingine kupoteza damu nyingi wakati wa kujifungua jambo linalosababisha kifo. Amesema kuna swala la umbali wa vituo hasa katika huduma za upasuaji nayo imekuwa moja ya changamoto ya kukabiliana na vifo vya uzazi. Amesema swala hilo pia linahusisha ubovu wa barabara hasa wakati wa masika na uhaba magari katika vituo vya afya. Amesema vituo vya afya Mbuga nyekundu, Kambi ya simba vina magari lakini Oldean bado hakuna gari. Amesema wanaendelea kukarabati jengo la upasuaji (theater) Mbuga nyekundu na kituo cha afya Endabash upasuaji utaanza mwezi wa kumi mwaka huu. Dkt Mustafa amesema ucheleweshaji ndani ya vituo, kwa mama mjamzito kupata huduma nayo imekuwa ni sababu ya vifo vya uzazi. amesema kunasababishwa na kukosekana kwa vifaa, kukosekana kwa mtoa huduma katika vituo vya afya au uzembe kwa watoa huduma. Taarifa zote za vifo za vinavyosababishwa na uzazi zinaripotiwa na zinajadiliwa ndani ya muda wa saa 48 ili sababu zilizosababisha zisijitokeze tena.
Dkt. Mustafa amesema sababu hizo tatu ndio lengo la kuzindua kampeni ya “JIONGEZE, TUWAVUSHE SALAMA TUPUNGUZE VIFO VITOKANAVYO NA UZAZI” . Dkt. Mustafa amesema hakuna tatizo la benki ya damu, amesema Karatu inaongoza kwa uchangia chupa 1250 kwa mwaka uliopita. Amesema hakuna kituo chchote cha afya kinachouza damu kwa mgonjwa. Amesema mwaka huu vifo vya kinama kuanzia January mpaka mwezi wa June, vifo vya wazazi ni viwili na vifo vya watoto wachanga vilikuwa 11. Dkt. Mustafa amesema wao kama wadau wa afya wanajitahidi kupunguza vifo hivyo, ndio maana wamezindua kamapeni hiyo.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa