Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo ameendelea na ziara yake wilayani Karatu. Ziara hiyo iliyoingia katika siku ya nne ametembelea soko la kuu la Karatu, ambalo ujenzi wa kuezeka bado unaendelea.
Mhe. Gambo amesema haridhishwi na kasi ya ujenzi wa soko kuu la mjini Karatu, ujenzi wa soko hilo ulianza mwezi 30/5/2018 na kutarajiwa kukamilika mwisho wa mwezi wa 8 mwaka 2018. Amesema tayari miezi mitatu iliyokusudiwa imeshaisha na sasa mwaka umepita, wananchi wameendelea kujibana kwa muda katika maeneo yasiyo rasmi kwa biashara wakitegemea serikali iwatengenezee maeneo mazuri zaidi ya kufanya biashara.
Mhe. Gambo amesema kitendo cha jengo hilo kutumia mchoro wa ramani ya pili baada ya ile ramani ya kwanza kimeonesha mapungufu ya kiutaalam. Amesema dosari hiyo imeweka mashaka juu ya uwezo wa mhandisi wa wilaya katika utendaji kazi. Mhe. Gambo amemuelekeza Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya ya karatu kumuondoa katika nafasi yake mwandisi huyo na kutafuta mhandisi mwingine kujaza nafasi yake kwa kushirikiana na katibu tawala wa mkoa.
Mhe. Gambo amesema mtu wa manunuzi wa Halmashauri, naye pia hajaweka mbele maslahi ya umma na wamefanya uzembe katika utendaji kazi. Mhe. Gambo amesema Halmashauri imelipa fedha bila kuona vifaa vinavyonunuliwa, utaratibu unaagiza vifaa na vifaa vikishafika vinakaguliwa na mkiridhika mnalipa. Halmashuri imelipa zaidi ya million 100 na vifaa vingine bado havijafika eneo la ujenzi. Amesema bado hata vifaa vilivyofika wataalam wamekiri vilikuwa na matatizo hivyo kurudishwa tena. Ametoa maelekezo ya kusimamishwa kazi kwa afisa manunuzi na kumuelekeza katibu tawala wa mkoa kuuunda timu ya uchunguzi katika ujenzi wa soko kuu la mjini Karatu. Mhe. Gambo ametoa muda mpaka 15/10/2019 soko kuu la Karatu liwe limekamilika kabisa na kuanza kutumika.
Awali katika taarifa yake mbele ya mkuu wa mkoa mhandisi Venance Malamla amesema mradi huo wa ujenzi wa soko ulikadiriwa kutumia million 540. Halmashauri kutokana na upungufu wa fedha imegawa ujenzi wa soko katika awamu mbili, awamu ya kwanza itagharimu shilingi million 222. Mhandisi Malamla amesema katika awamu hiyo ujenzi ulihusisha nguzo na kupauwa jengo lote. Hatua ya pili ya ujenzi ni kujenga sakafu; vizimba, kujenga ukuta wa nje na kuweka miundo mbinu ya maji na moto. Utaratibu wa kujenga soko hilo unatumia force account, mradi huo unatekelezwa na fundi Anatory construction limited akiletewa vifaa na kusimamiwa na wataalamu wa Halmashauri.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa