NA TEGEMEO KASTUS
Watumishi wanapaswa kutekeleza majukumu ya kikazi kwa kufuata mfumo kazi taarifa (Database) katika maeneo yao ya kazi. Mfumo kazi taarifa ulioandaliwa kitaalamu unamuwezesha mtumishi wa umma kujua mahitaji muhimu katika eneo lake la kazi na kufahamu eneo lenye mapungufu na eneo ambalo limeimarika katika kutoa huduma.
Naibu Katibu Mkuu Afya (Tamisemi) Dkt. Dorothy Gwajima amesema hayo katika ziara ya siku moja alipotembelea kituo cha afya Karatu na kuzungumza na CHMT. Shida kubwa ya watumishi wa afya hawatumii na hawaandai mfumo kazi taarifa ili kujua hali ya vituo vya afya. Amesema hali hiyo imechangia sekta ya afya kutofanya kazi kwa ufanisi hasa katika kutoa huduma za afya. Amesema kumekuwa na mtizamo uliojengwa kwamba sekta ya afya ni sekta ya madaktari na wauguzi tuu basi. Mtizamo ambao unazidi kuididmiza sekta ya afya badala ya kuijenga ili izidi kufanya kazi kwa ufanisi.
Dkt. Gwajima amesema sekta ya afya haiwezi kukaa yenyewe tuu basi lazima wataalamu wengine washiriki katika usimamizi mathalani katika afya kuna uchumi lazima mtu wa uchumi atoe utaalamu wake ili kuinua sekta ya afya. Lazima Mtunza hazina wa Halmashauri aweze kusimamia mapato yanayotokana na sekta ya afya ikiwa ni pamoja na kuangalia ufanisi wake. Ameongeza kusema lazima Mkaguzi wa ndani akague mapato na matumizi ya sekta za afya katika vituo vyote kwa kuangalia taratibu zilizofanywa katika ufanyaji wa malipo.
Dkt. Dorothy Gwajima ( kushoto) akimjulia hali mama aliyelazwa wodi ya wazazi katika kituo cha afya Karatu, alipokuwa akikagua hali ya utoaji wa huduma katika kituo hicho.
Dkt. Gwajima amesema lazima sekta ya afya ihusishe mtu wa manunuzi katika kufanya taratibu za ununuaji wa dawa na vifaa tiba katika vituo vya afya. Ameongeza kusema kama unataka kununua kitu lazima Afisa Manunuzi ahusishwe lakini pia aombe Inventory report ya afya kabla hujafanya maamuzi. Madhara ya kununua vitu bila kufanya tathimini ni kuleta hasara kwa serikali. Amesema sekta ya afya inapaswa iwe sekta ya kusaidia kujenga uchumi wa nchi badala ya kuwa sekta tegemezi. Ameongeza kusema sekta ya afya inamhitaji mtu wa Mipango wa kuchanganua mambo yote yanayofanyika katika sekta ya afya na kuyawekea mikakati ya utekelezaji kwa kujumisha wataalamu mbalimbali. Hivyo ndivyo sekta ya afya inapaswa kwenda badala ya kufanya mambo wenyewe wenyewe tuu.
Dkt. Gwajima amesema Afisa utumishi ni mtu muhimu sana kwenye sekta ya afya yeye ndiye anaye fahamu muuguzi mmoja anatakiwa kuhudumia wagonjwa wangapi?? Medical Doctor anatakiwa awe anawastani wa kuwahudumia wagonjwa wangapi katika kituo. Hayo yote Afisa utumishi anaweza kuyafanyia kazi kama kuna kazi taarifa zilizochambuliwa kitaalamu, na kwa kupitia taarifa za kitaalamu ni rahisi Afisa utumishi kujua nani awe mfanyakazi bora na nani awe Promoted (kupandishwa daraja la kiutumishi)
Amehimiza watu wa afya kuichukulia kazi yako kama mkombozi wa wananchi wanyonge, mtu anapokuja kwenye kituo cha kazi lazima umuhakikishie unampa tumaini jipya. Lazima mtumishi uonyeshe thamani kubwa katika ufanisi wa utendaji kazi ili hata Muajiri aogope kukupoteza. Hayo yanawezekana kama unaweza kufanya kazi kwa kuiunganisha na imani ya kiroho katika maono ya kimungu.
Dkt, Gwajima akizungumza na watendaji wa kituo cha afya Karatu
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa