Na Tegemeo Kastus
Wananchi wa kijiji cha Getamock wamepongezwa kwa moyo wao wa kizalendo wa kujitolea nguvu kazi katika ujenzi wa miradi ya maendeleo. Wananchi hao wamejenga daraja dogo la mawe lilojengwa na wananchi katika kijiji cha Getamock ili kuimarisha mawasiliano ya kuingia na kutoka na limegharimu kiasi cha shilingi million mbili.
Mh. Kayanda akiwa katika daraja lilojengwa na wananchi wa kijiji cha Getamock
Hayo yamesema na Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Abbas Kayanda alipokuwa akizindua mradi wa daraja la Gendaa-Getamock. Ujenzi ambao umeondoa adhaa ya usafiri kipindi cha masikia kwa wananchi wa vijiji vya Getamock na Mahhahha ambao walikuwa wakilazimika kusubiri kwa muda mrefu mpaka maji ya mvua yapungue kwenye korongo ili waweze kuendelea na safari kwa kuvuka upande wa pili.
Mh. Kayanda amepongeza serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mh. Rais. Samia Suluhu Hasani kwa kutoa fedha kiasi cha billion 2.5 kwa mwaka wa fedha 2021-2022 wilayani Karatu. Ujenzi wa daraja Gendaa-Getamock umegharimu kiasi cha shilingi million 52,722,904, amesema serikali inatumia gharama kubwa katika ujenzi wa miundo mbinu ya barabara, hivyo wananchi wanapaswa kutunza miundo mbinu. Mh. Kayanda amekemea tabia za watu wasio waadilifu wanaojihusisha na kukata chuma zinazozunguka kingo za daraja. Amesema tabia hizo zinarudisha nyuma juhudi za ujenzi wa miundo mbinu ya barabara. Ametoa wito kwa wananchi kusimamia na kuhifadhi vizuri miundo mbinu ya barabara na maji iliyojengwa ili iweze kudumu na kuhakikisha wanatoa taarifa za vitendo vya uharibifu wa miundo mbinu ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa kwa wahusika.
Mh. Kayanda akizindua daraja la Gendaa-Getamock
Katika hatua nyingine Mh. Kayanda ametembelea na kujionea ujenzi wa daraja la Endala ambao serikali kupitia wakala wa barabara vijijini Tarura imetoa kiasi cha shilingi million 599 na tayari mkandarasi wa daraja hilo ameshaanza kazi. Ujenzi wa daraja hilo la Endala inasimamiwa na kampuni ya Zowange na unatarajiwa kukamilika mapema mwezi wa kumi na mbili mwaka huu.
Wakati huo huo Mh. Kayanda amezindua mradi wa maji wa vijiji vya Getamock na Mahhahhaa uliokuwa ukifanyiwa marekebisho sehemu korofi zilizoathirika takribani mita 8900. Ukarabati ulihusisha tank la maji na vilula 22 na kujenga vilula 4 kwa kiasi cha cha million 82782131. Mradi huo unauwezo wa kutoa huduma kwa wakazi 11000. Mh. Kayanda amesema mradi wa maji Geatmock na Mahhahha ni wa muda mrefu, serikali imeukarabati ili kuboresha na kusogeza huduma za maji karibu na wananchi wa vijiji vya Getamock na Mahhahha.
Mh kayanda akikagua mradi wa maji katika kijiji cha Mahhahhha
Amesema serikali imedhamiria kumtua mama ndoo kichwani hivyo itamalizia urekebishaji wa sehemu ya miundo mbinu ya maji iliyobakia katika mradi. Mh. Kayanda ametoa rai kwa wananchi kuilinda miundo mbinu ya maji kwa kutoa taarifa za watu wasio wema wanaojihusisha na kukata mabomba ya maji.
Awali mwenyekiti wa kijiji cha Getamock Ndg. Jeremia Boay amesema pamoja na ukarabati wa uliofanywa na serikali katika kuboresha huduma ya maji, bado serikali ya Halmashauri ya kijiji itakaa ili kuona inavyoweza kujitoa katika kukarabati sehemu ya miundo mbinu maji wakati ikisubiri serikali. Amesema ukarabati wa maeneo yaliyobakia ni muhimu sana katika kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji.
Naye Mwenyekiti wa kijiji cha Mahhahha Ndg. Samweli Ammi amesema wanaishukuru serikali kwa kuboresha miundo mbinu ya maji. Amesema ukarabati huo umewaondolea shida ya kuchota maji kwenye Makorongo.
Mh. Kayanda akizindua mradi wa maji kijiji cha Mahhahha.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa