Shirika lisilo la kiserikali la (JIVITA) Jitegeeme vijana Tanazania foundation; limetoa taulo za kike kwa vijana wa kike walio shuleni katika wilaya ya Karatu. Msaada huo ni jitihada za kumsaidia mtoto wa kike kutimiza ndoto zake.
Bi, Yasinta Lekule Afisa vijana wa Jivita; amesema katika mradi wa kugawa taulo unaoitwa Mwanao, wameweza kusambaza taulo za kike 1632 ndani ya wiki moja kwa shule 9 za serikali wilayani Karatu. Bi Yasinta amesema kila mtoto amepata taulo moja na lengo ni kusambaza taulo kwa vijana walio shuleni wenye uhitaji. Zoezi hilo limefanyika katika ukanda wa kata ya Kansay Tarafa ya Endabash na baadhi ya shule katika tarafa ya Karatu. Amesema lengo la shirika hilo ni kutoa msaada kwa wilaya nzima, awali walianza zoezi hilo kwa kugawia vijana wa kike katika tarafa ya Eyasi.
Bi, Yasinta amesema, “lengo ni kumwezesha mtoto wa kike kutimiza ndoto zake.” Kijana wa kike lazima ajisitiri vizuri wakati anasoma. Amesema vijanawa kike wenye uhitaji hukosa masomo kwa kutohudhria shule kwa kuhofia kuadhirika pindi wanapokuwa kwenye mzunguko wa hedhi.Amesema zoezi hilo ni endelevu na wanatarajia kuja mwezi wa kumi kusaidia tena vijana wenye uhitaji.
Shirika linajihusisha na Mradi wa Sio Mwisho, ambao nao umejikita katika kuwawezesha watoto waliokosa shule kwa kuwapatia huduma muhimu. Bi, Yasinta amesema wana jihusisha na watoto waliokosa shule ambao wanaishi mtaani, wao kama Jivita wanawasaidia kurudi nyumbani na kuwashawishi kuendelea na masomo au kusoma kitu anachokipenda. Amesema wanafanya shughuli zote hizo kupitia wafanyabiashara wa mjini Arusha wanaotoa misaada mbalimbali kwa ajili ya vijana hao. Amesema kwa sasa wanafanya shughuli hizo katika mji wa Arusha, lakini wataongeza wigo wa kazi zao kwa wilaya nyingine.
Bi, Yasinta amesema shirika lao limejikita katika shughuli za mazingira, amesema mabadiliko ya nchi yanaathari kubwa sana katika shughuli za utalii. Shirika limezindua kamapeni ya Nitunze Mazingira, Mazingira Yakutunze ambayo itazinduliwa mkoani Arusha 14/Oct/2019. Amesema kuelekea wiki ya kilele cha siku ya utalii; tumepanda miti 300 kwa kushirikiana na shirika la TAJPI kwa shule za serikali za sekondari na msingi. Amesema malengo yao ni kuzuia athari za kimazingira zinazochangiwa na utunzaji mbovu wa mazingira.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa