Kikao cha baraza la madiwani Halmashauri ya wilaya ya Karatu cha robo ya kwanza ya Mwaka wa fedha 2019-2020 kimekaa na kujadili taarifa za maendeleo za kata. Kikao hicho kimeongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Emmanuel Gege.
Mhe. Elias Simpa diwani wa kata ya Mbulumbulu amesema katika taarifa yake kwamba wananchi wa kata ya Mbulumbulu wanapata changamoto ya kutopata huduma ya maji safi kipindi cha kiangazi kwa sababu maji wanayotegemea kwa matumizi ya manyumbani yanatoka chanzo cha hifadhi ya Ngorongo. Maji huwa yamechafuka kwa sababu wananchi wa maaeneo mengine hunywesha mifugo katika vyanzo vya maji hivyo kuathiri wananchi wa ukanda wa chini wanaotegemea maji ya matumizi ya manyumbani kutoka katika hifadhi ya mamlaka ya Ngorongoro.
Mhe. Elias Simpa amesema kwa upande wa kata ya Mbulumbulu wao wameelimisha wanaanchi umuhimu wa kuhifadhi vyanzo vya maji na wameelewa. Ameomba baraza la madiwani la Halmashauri ya wilaya Karatu kulipa msukumo swala hilo ili wananchi wa maeneo mengine wanaozunguka chanzo hicho waone umuhimu wa kuhifadhi vyanzo vya maji. Adha wanayopata wananchi wa kata ya Mbulumbu ni pamoja na wakati mwingine kulazimika kutumia maji ya rangirangi kutokana na mifugo kutifua na kuvuruga vyanzo vya maji.
Watendaji wa Halmashauri ya Karatu wakiwa katika kikao cha baraza la madiwani.
Naye Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Simon Bajuta amesema tayari wameshakaa vikao vya ujirani mwema kati yao na mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro madiwani wa Halmashauri ya Ngorongoro na Monduli kujadili swala hilo kwa kina ili kuja na ufumbuzi wa pamoja wa changamoto hiyo. Amesema wamekubaliana katika kikao hicho kwamba wananchi wasinyeshwe mifugo katika vyanzo vya maji.
Afisa wanyamapori wa wilaya ya Karatu Bi, Donata Kimario amesema wilaya ya Karatu imepakana na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro. Amesema msitu wa nyanda za juu kaskazini umehifadhiwa kwa ajili ya wanyama na vyanzo vya maji. Eneo hilo linalindwa na mamlaka ya hifadhi ya ngorongoro, ameomba mamlka hiyo kuongeza ulinzi katika vyanzo vya maji ili wananchi wasitumie kunywesha mifugo katika maeneo ya vyanzo vya maji ili kuepeuka uchafuzi wa maji yanayotegemewa kwaajili ya matumizi mbalimbali ya nyumbani
Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe.Emmanuel Gege amesema maji ya Manyumbani wanayotumia wananchi wa Wilaya ya Karatu, vyanzo vyake vinatoka hifadhi ya mamlaka ya Ngorongoro. Amesema wao wanaamini katika mazungumzo ndio maana wanakaa vikao vya ujirani mwema ili kuja na ufumbuzi wa kutatua swala hilo kwa pamoja.
Madiwani wakiwa katika kikao cha robo ya kwanza cha baraza.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa