Mkuu wa mkoa wa arusha Mhe. Mrisho Gambo amefanya ziara katika wilaya ya Karatu. Katika ziara yake ametembelea eneo la kitalu K katika mtaa wa Bonite mjini Karatu. Eneo la kiwanja lina mvutano kati ya wananchi waliokuwa wanaishi katika eneo hilo na Halmashauri ya wilaya ya Karatu.
Mhe. Gambo alipata nafasi ya kusikiliza pande zote mbili katika mgogoro huo. Amesema kabla ya kupanga safari hiyo alituma timu kuchunguza mgogoro huo ambao imeshampa taarifa. Mhe. Gambo amesema ameona nyaraka za Halmashauri za kuonesha historia ya eneo hilo. Ametoa wiki moja kwa wananchi kutoa nyaraka zao na kuzipeleka kwa mkuu wa wilaya ili Mhe. Gambo aweze kuangalia pamoja na hizo za Halmashauri, na mwisho ataandika taarifa juu ya jambo hilo. Amesema kama kuna mtu anamiliki eneo hilo, afuate sheria kwa kwenda mahakamani ili apewe amri ya kuwaondoa watu katika eneo husika.
Mkuu wa Wilaya ya Karatu Mhe.Theresia amesema eneo hilo lenye mzozo lilikuwa la Halmashauri. Eneo hilo la (Veterinary) lilikuwa la kuoshea mifugo awali, Madiwani wa wakati huo waliamua kulipima eneo hilo. Wakabadilisha matumizi ya eneo la Veterinary kwenda kwenye matumizi ya biashara. Wakatangaza eneo hilo, watu wakaomba wakagawiwa, hata mmiliki wa eneo hilo wa sasa naye alinunua kwa mtu aliyemilikishwa na madiwani wa Halmashauri. Mhe. Theresia amesema yeye amekuta vibanda vitatu, viwili vilikuwa vinatumika kama makazi. Mhe Theresia amesema kweli wafanyabishara hao walitolewa eneo moja la biashara kuja eneo hilo lenye mzozo sasa kwa ajili ya kufanya biashara kwa mda. Amesema ili wananchi hao wapate haki alimuelekeza Mkurugenzi wa Halmashauri kuwapatia eneo jingine la kufanya biashara.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndugu Waziri Mourice amesema wafanyabishara hawa walikuwa wanafanya bishara ndogondogo pembezoni mwa barabara. Waliondolewa katika maeneo yao ya bishara kupisha ujenzi wa barabara, hivyo kuhamishiwa kwa mda eneo hilo la kitalu K, Mtaa wa Bonite. Eneo hilo la kitalu ‘K’ liliuzwa kwa mtu kwa kufuata sheria na taratibu zote za serikali. Baada jambo hilo kuleta mgogoro kwa watu waliokuwa wakiishi hapo kwa mda, Halmashauri iliwatafutia eneo jingine kwa mkataba maalumu la kufanya biashara. Watu waliohamishiwa katika eneo la kitalu ‘K’ kwa muda wako 31 baada ya kuona kuna watu wengine ambao walimuomba mumiliki halali wa eneo hilo wafanye bisahara, Halmashauri iliamua kuwajumuisha nao kwa kuwapa maeneo mengine hivyo kufanya idadi kufika watu 35.
Mwananchi (ambaye hatukupata jina lake) aliyejenga nyumba ambaye analalamika kubomolewa choo pamoja na eneo hilo kuzungushiwa. Amesema vibanda vingine vilivyokuwa katika kitalu ‘K’ vimebomolewa na wao hawana sehemu ya kufanya kazi. Amesema wamekuwa wakienda polisi lakini hawasikilizwi, amesema yeye amehamia mwaka 2000 mwezi wa tatu kutoka ng’ambo ya lami. Amesema ananyaraka inayosema watu kutoka ng’ambo ya barabara wahamishwe na Halmashauri iliwaleta hapo. Mkazi huyo anasema wakati wanahamia maeneo hayo waliambiwa hayajapimwa lakini yatakapopimwa eneo hilo litakuwa la kwao na litaitwa soko Mjinga.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa