Watumishi wa idara ya afya waanze utaratibu wa kubandika kwenye vituo vya afya dawa zinazopatikana. Ili kumsaidia mwananchi anapoenda zahanati au ngazi ya kituo cha afya kujua ni dawa za aina gani zinapatikana, kuainisha aina za dawa itasaidia kuondoa malalamiko kwa wananchi kwamba vituo vya kutolea huduma za afya havina dawa.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh.Abbas Kayanda wakati alipotembelea zahanati ya Dofa kujionea hali ya utoaji wa huduma na upatikanaji wa dawa. Amesema wananchi wanapaswa kufahamu katika ngazi ya zahanati dawa za aina gani zainapatikana, ngazi ya kituo cha afya dawa za aina gani zinapatikana ili kujenga uelewa wa pamoja.
Mh. Abbas Kayanda (kushoto) akikagua hali ya upatikanaji wa dawa katika kituo cha afya Dofa
Mh. Kayanda amewalekeza watumishi wa idara ya afya kuhakikisha huduma katika vituo vya zinaboreshwa na kuzingatia kuweka mazingira rafiki ya kutolea huduma. Mh. Kayanda amesema chumba cha uzazi, chumba cha sindano chumba cha kusafisha majeraha ya vidonda lazima viwe na faragha inayomuwezesha mgonjwa kusitirika wakati akipata huduma. Badala ya utaratibu wa sasa ambao vyumba hivyo havioneshi namna ya kumsitiri ugonjwa wakati akipewa huduma.
Katika hatua nyingine Mh. Abbas Kayanda amewaelekeza watendaji wa vijiji na kata kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko wa bima ya afya iliyoboreshwa ili kuongezea kituo uwezo wa kupata dawa. Amesema idadi ya wakinama wanaojifungulia hospitali ni ndogo jambo hilo linatokana na mwamuko kuwa mdogo kwa wananchi. Lazima jitihada za kuelimisha wananchi kujifunglia hospitali ziongezwe ili wananchi wahamasike kupata huduma katika vituo vya afya.
Mh. Kayanda amesema hata supervision zinazofanyika na wataalam wa afya lazima zilete matokeo chanya. Taarifa za ukaguzi ziwe ndio sehemu ya kujitathimini utendaji wa watumishi vituo vya afya ili kuja na njia za kuboresha huduma za afya.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa