Kikao cha kawaida cha baraza la madiwani kimekaa leo katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Karatu. Kikao hicho cha robo ya tatu ya mwaka kimeongozwa na Mwenyekiti wa baraza la madiwani Mhe. Jublate Mnyenye.
Kikao hicho kiliwapa nafasi waheshimiwa madiwani kutoa taarifa za maendeleo za kata kwa kipindi cha miezi mitatu iliyopita. Sambamba na hilo pia madiwani walihoji uhalali wa taarifa za kata, ambazo madiwani wao wamejiuzulu na hazikuwa na uwakilishi wa madiwani.
Mwanasheria wa Halmashauri Ndugu Prosper Ndomba alieleza mbele ya baraza la madiwani tafsiri ya kanuni kisheria. Kanuni ya ishirini na tano, kanuni ndogo ya pili inasema taarifa za utekelezaji wa kata zitawasilishwa na diwani wa kata husika, na kama diwani huyo hayupo itawasilishwa na diwani wa viti maalumu anayeishi katika kata hiyo, na kama diwani wa viti maalumu hayupo, Mwenyekiti atamtaarifu mapema diwani mwingine yeyote asaidie kuwasilisha taarifa hiyo. Ndugu Ndomba amesema taarifa zinaletwa ili kama kuna hoja au swala la ufuatiliaji liende kwenye kamati husika. Hakuna hofu ya kuwasilisha taarifa na wala muwasilishaji habanwi kujibu taarifa ya kata husika.
Mhe. Jublate ameomba waheshimiwa madiwani kuendelea kuhamasisha wananchi kujiunga katika mfuko wa bima ya afya iliyoboreshwa. Elimu iendelee kutolewa kwa wananchi wengi, ili wajitokeze kujiandikisha na wapate bima ya afya. Mhe Jublate amesema mambo yamebadilika bima ya afya ni swala muhimu sana, gharama za matibabu zipo juu. Serikali hutoa msaada kwenye maeneo ambayo wamefika zaidi ya 25% ambayo serikali inachukulia kama kiwango cha chini. Amesema ili serikali iweze kutoa top up ya 25% lazima tufike kiwango cha chini cha serikali. Mhe. Jublate amesema Karatu haijafika kiwango cha 25% ili kuweza kunufaika na (top up ) fedha za serikali.
Waheshimiwa madiwani katika kikao cha baraza la madiwani.
watendaji wa Halmashauri katika baraza la madiwani.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa