Na Tegemeo Kastus
Wakuu wa shule za sekondari mkoa wa Arusha wamehimizwa kuimarisha umoja katika kufanya kazi katika maeneo yao ya kazi. Hiyo itasaidia kubadilishana uzoefu na kuongeza maarifa na weledi wa kuongoza shule na kuinua kiwango cha ufaulu wa wanafunzi.
Mh. Abbas Kayanda amesema hayo wakati akifungua mkutano wa (TAHOSSA) Tanzania heads of secondary schools associations wa mkoa wa Arusha katika ukumbi wa Karatu secondary. Amesema Tahossa inatakiwa kusimama vizuri katika ngazi ya wilaya kwa sababu vikao vinavyofanyika Mkoani vya Tahossa, watekelezaji wake wakuu wapo katika ngazi ya wilaya. Vikao vya aini hii vikiwepo kwenye wilaya itasaidia kuimarisha vikao vya mkoa. Tunahitaji kuona mkoa wetu ukiendelea kupiga hatua katika kuongeza ufaulu wa wanafunzi kitaaluma.
Mh. Abbas Kayanda katika matukio tofauti wakati akihutubia walimu kwenye kikao cha wakuu wa shule Mkoa wa Arusha
Ameongeza kusema umoja wa walimu wakuu wa sekondari Tahossa ni daraja linalowakutanisha na viongozi wa serikali. Lazima tuongezee idadi ya washiriki katika mikutano ya Tahossa katika ngazi ya wilaya ili kuibua maoni na changamoto ambazo zitaletwa ngazi ya mkoa na kufikishwa serikalini.
Mh. Kayanda amechukua nafasi hiyo kuwapongeza walimu wakuu kwa matokeo mazuri waliyoyapata kitaaluma katika mkoa wa Arusha. Amesema kwa ujumla tufanya vizuri kitaaluma lakini tukifanya tathimini ya wilaya moja moja na shule moja moja bado hali si nzuri. Amesema jukwaa hilo litumike kupeana maarifa ili kupata namna nzuri ya kuongeza kiwango cha ufaulu. Mkoa wa Arusha umeshika nafasi ya kwanza kwa ufaulu mzuri wa kitaaluma lazima tuje na mkakati wa kutunza kiwango cha ufaulu wa wanafunzi katika shule zetu.
Wakuu wa shule wakimsikiliza Mh. Abbas Kayanda wakati wa hotuba ya ufunguzi
Akizungumzia kuhusu nidhamu Mh. Kayanda amesema lazima walimu tuendelee kuchukua hatua za kusimamia nidhamu kwa wanafunzi, swala la nizamu haliishii kwa wa wanafunzi peke yao. Amesema mwalimu lazima avae mavazi yenye staha, mwalimu mkuu lazima awe na fikra pevu katika utendaji wa kazi. Ameasa walimu katika vikao vya ndani vya shule kuacha kuoneana aibu kwenye utendaji usioridhisha na badala yake kujikita katika kujenga msingi mizuri ya kiutendaji. Amesema mtumishi yeyote anapaswa kuwa na nidhamu katika maisha binafsi na anapaswa kuwa nidhamu katika sehemu ya kazi.
Ameongeza kusema Mwalimu Mkuu hapaswi kuwa kiongozi wa kuwagawa walimu, Mwalimu Mkuu anatakiwa kujenga jumuiya yenye umoja sehemu ya kazi. Mwalimu mkuu ni kiongozi anayepaswa kulea badala kutenga watu, walimu tupendane katika misingi ya kazi. Walimu tunapaswa kusaidiana wenyewe kwa wenyewe, hatupaswi kuoneana wivu wa maisha, amesema maisha ni mipango. Walimu tunapaswa kushirikiana katika hali zote ili mwisho wa siku tuwe na mafanikio yenye kulingana.
Akizungumzia kuhusu kuongeza kiwango cha ufaulu, Mh. Kayanda amesema katika kuinua ufaulu kuna mbinu nyingi za kufanya ili kuongeza ufaulu. Amesema mkoa wa Arusha una utaratibu wakufanya mtihani wa pamoja wa kimkoa amesema ni vyema kutengeneza utaratibu wa kufanya mitihani ya pamoja katika ngazi ya wilaya. Amesema ni wakati sasa wakuja na mkakati wa kutokomeza divison zero.
Akitoa salamu za shukrani Mwalimu mkuu John Silvan Massawe wa shule ya sekondari ya Mwandet wilaya ya Arusha, amesema wanapambana usiku na mchana kuendelea kuilinda nafasi ya kwanza kitaaluma waliyoipata. Amesema kikao cha Tahossa kimelenga kuandaa mikakati mipya ya kuinua ufaulu wa kitaaluma. Amesema wanafahamu fika kitendo cha Mkoa wa Arusha kuwa wa kwanza kwa ufaulu kitaaluma kuna watu watataka kutupita, amesema wanajipanga vizuri kuilinda nafasi yao.
wakuu wa shule Mkoa wa Arusha katika matukio fofauti wakati wa kikao
Akizungumzia kuhusu nidhamu Mwl Massawe amesema kuna shida ya malezi kwa vijana wa kizazi cha sasa, amesema kwa sababu walimu wakuu ni walezi wataendelea kuwaelekeza walimu namna nzuri za kutekeleza majukumu yao wakiwa katika maeneo ya kazi. Ameomba vyuo vya ualimu kuhimiza misingi ya maadili ya ualimu katika Vyuo.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa