NA TEGEMEO KASTUS
Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa wilayani Karatu imeokoa kiasi cha million 21 na laki moja kwa Mwalimu Mstaafu. Fedha hizo zilikuwa zimeporwa na kampuni ya Robby credit Company limited inayomilikiwa na Emmanuel Bonifasi tangu February Mwaka 2019.
Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Abbas Kayanda amesema Mzee Pilonga Vicent alienda kukopa fedha kwenye taasisi ya kifedha ya Robby credit kiasi cha million 3 kwa makubaliano ya kurudisha kiasi cha fedha hizo na riba ya 30%. Amesema baada ya kuingia kwa fedha yake ya kusataafu million 25 fedha zote zilichukuliwa na taasisi ya Robby credit.
Mh. Kayanda amesema vyombo vya habari vimemsaidia kujenga elimu ya uelewa Mzee Pilonga juu ya namna taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa inaweza kumsaidia. Amesema Takukuru walichunguza kwa undani jambo la Mzee Pilonga na kugundua kwamba taasisi ya Robby credit ilichukua kadi ya bank na pamoja na numba yake ya siri. Amesema hiyo ilichangia fedha za Mzee Pilonga kuchukuliwa na taasisi ya Robby credit.
Mh . Kayanda amesema watendaji wa Takukuru walilisimamia jambo hilo na viongozi wa Robby credit walikiri makosa waliyoyafanya na kurudisha fedha hizo. Mh. Kayanda ametoa wito kwa wananchi ambao wamedhulumiwa katika taasisi za kifedha na wanaushahidi wawasilishe malalamiko katika taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa. Amesema hata wananchi wanaoenda katika taasisi za umma kupata huduma, kama kuna vitendo vyovyote vinavyoashiria rushwa wasisite kutoa taarifa Takukuru ili kudhibiti vitendo vinavyoharibu taswira ya utendaji kazi.
Awali katika taarifa yake Naibu wa takukuru Arusha Sabasi Salehe amesema matatizo hayo yamezidi kuongezeka mkoani Arusha. Amesema wameanza kurejesha fedha nyingi, amesema hushughulikia watuhumiwa kwa njia mbili kwanza kwa kuchunguza kwa kina na kujiridhisha kama Mtuhumiwa aliyefanya alifanya pasipokujua, kama ni kweli akirejesha fedha alizochukua anasamehewa na kuonywa. Amesema kuna watuhumiwa ambao wanavunja sheria ya Takukuru No1 ya mwaka 2017 hivyo sheria inachukuliwa dhidi yao.
Mh. Abbas Kayanda (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mzee Pilonga pamoja na maafisa wa Takukuru
Kamanda wa Takukuru wilaya ya Karatu Bi. Atuganile Stephen amesema wananchi wenye mikopo umiza watoe taarifa ofisini ikiwa ni pamoja na watu wenye taarifa za vitendo vya rushwa. Amesema jukumu la kupambana na rushwa ni letu sote .
Naye mtaafu aliyerejeshewa fedha zake Mzee Pilonga amesema anajisikia amani yake imerejea kwa sababu alikuwa anawaza analeaje familia kutokana na unyang’anyi aliofanyiwa. Amesema lakini kutokana na juhudi za serikali kupitia Takukuru fedha zake zimepatikana, Mzee Pilonga ameishukuru sana serikali kwa msaada aliopata.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa