NA TEGEMEO KASTUS
Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa wilayani Karatu imeokoa kiasi cha million 56.7 zilizokuwa zimefanyiwa ubadhilifu. Fedha hizo zinajumuisha makundi mbalimbali ikiwemo mapato ya serikali, vyama vya ushirika, SACCOS na watu binafasi.
Akizungumza wakati wa urejeshwaji wa fedha hizo Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Abbas Kayanda amesema serikali ya awamu ya tano ikiongozwa na Mh. Dkt John Pombe Magufuli tangu imeingia madarakani imejikita katika kupambana na rushwa. Serikali inasimamia haki ndio maana fedha hizi zinarejeshwa, Mh. Kayanda amewapongeza Takukuru kwa kazi nzuri waliyofanya.
Akizungumzia fedha za vitambulisho vya wamachinga zilizorejeshwa Mh. Kayanda amewaasa watumishi wa serikali na hasa watendaji wa Halmashauri kuhakikisha wanasimamia majukumu yao kwa uaminifu bila kufanya ubadhilifu. Kiasi cha million 19.5 za vitambulisho vya wamachinga vya awamu ya kwanza ambazo zilikuwa zimepotea zimepatikana baada ya Takukuru kufanyia kazi taarifa ubadhilifu wa fedha hizo. Mh. Kayanda amesema vitendo vya namna hiyo ni vitendo ambavyo havifai na nivitendo ambavyo vinaweza kumfanya mtumishi afukuzwe kazi.
Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Abbas Kayanda (kulia) akikabidhi fedha za ofis ya kijiji zilizookolewa na Takukuru kwa Katibu tawala wa wilaya ya Karatu Bi, Faraja Msigwa
Mh. Kayanda ametoa rai pia kwa watendaji vijiji kuheshimu fedha ambazo serikali inaleta kwa ajili ya miradi ya maendeleo. Lakini kuheshimu fedha ambazo wananchi wanachangia kwa ajili ya miradi ya maendeleo, fedha hizo lazima zitumike kwa kufuata utaratibu wa serikali. Amesema vitendo vya ubadhilifu wa fedha vikiachwa vikaendelea vitakuwa vinawavunja wananchi moyo katika kuchangia miradi ya maendeleo. Kiasi cha 2241,000 zimerejeshwa ambazo zilikuwa za ujenzi wa ofisi kijiji lakini pia kiasi cha 623,000 zimerejeshwa kwa ajili ya ujenzi wa sekondari ya Eyasi ambayo nazo zilifanyiwa ubadhilifu na uongozi wa kijiji.
Katika ushirika amesema serikali imedhamiria kuimarishwa ushirika lakini katika vyama vya ushirika vya wakulima wadogo wadogo SACCOS viongozi wao wamekuwa wakishirki kuhujumu vyama hivyo. Ametoa wito kwa viongozi wa vyama hivyo kujirekebsha nakuacha tabia za namna hiyo. Fedha ambazo wanachama wamechangia inapotakiwa kutumiwa lazima taratibu zifuatwe. Kiasi cha million 32, 793,847 ambazo kiasi cha 17,766,647 ilikabidhiwa saccos ya Mangola na 13,771,180 zimerejeswa mbulumbulu saccos baada ya wanachama na viongozi kujikopesha bila kurejesha kwa mujibu wa taratibu zilizowekewa. Fedha nyingine zilizorejeshwa ni fedha za AMCOS ya Gilala kiasi cha 125,6000 fedha ambazo wanachama na viongozi walijikopesha bila kufuata utaratibu jambo lilowanyima wanachama wengine nafasi ya kukopa.
Matukio mbalimbali katika picha Mh. Abbas Kayanda akikabidhi fedha zilizorejeshwa na Takukuru
Kuhusu swala la mikataba ya ajira Mh. Kayanda amesema katika kuajiri huwa kunakuwa na ajira za muda mrefu na ajira za muda mfupi. Ametoa rai kwa waajiri wote wa makapuni binafsi kuhakikisha wanatoa mikataba kwa watumishi wao. Mh. Kayanda amezungumzia hilo baada ya watumishi wa Usafi Group waliokuwa wanamdai muajiri wao kiasi cha 6000,00 kupewa fedha zao baada ya muajiri wa kampuni hiyo kuwaachisha kazi bila kuwalipa mishahara ya miezi miwili. Kiasi hicho cha fedha kimepatikana baada ya Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa kufuatilia swala lao kwa muajiri wa Usafi Group.
Mh. Kayanda amesema watu wa Takukuru wataendelea kukagua miradi mbalimbali ya mendeleo ili kujiridhisha kama miradi inayojengwa inaendana na thamani fedha zilizotolewa. Ametoa rai kwa wananchi kutoa taarifa zozote zinazohusiana na rushwa katika ofisi ya Takukuru ili hatua stahiki zichukuliwe haraka ili watu wapate huduma bila usumbufu. Hii itasaidia kuhakikisha mazingira yote ya utoaji wa rushwa yanadhibitiwa.
Kamanda wa Takukuru wilaya ya Karatu Bi, Atuganile Stephen amesema hakuna mtu aliye juu ya sheria, kama mwananchi anaona amedhulumiwa au kunyanyaswa katika kutafuta haki zake ni vyema akatoa taarifa Takukuru. Lakini pia kamanda wa Takukuru ameshukuru kwa ushirikiano wanaoupata kutoka ofisi ya Mkuu wa wilaya, ushirikiano ambao umesaidia kubaini mianya mingi ya ubadhilifu kwenye miradi ya maendeleo.
Nao wananchi waliorejeshewa Ndg. Paskali Safari na Samweli Bura wameishukuru serikali na Takukuru kwa kuwasaidia kurejesha fedha zao na kusimama pamoja nao katika kipindi cha kudai haki zao. Wametoa rai kwa wananchi wanapopata shida kama walizopata wao wasisite kutoa taarifa Takukuru au ofisi ya Mkuu wa wilaya.
Wananchi wanapaswa kukimbilia serikalini kupata msaada, wamesema wamefarijika kuona serikali imewasaidia kupata fedha zao bila kudai kiasi chochote cha fedha. Amesema jambo hilo limezidi kuwajengea imani na Taasisi ya Takukuru na serikali kwa ujumla.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa