Tamasha la utamaduni la urithi limefanyika kwa siku tano mfululizo na jana ilikuwa siku ya mwisho kwa wilaya ya karatu. Karatu ndio wilaya pekee iliyopata nafasi ya kuandaa tamasha hilo. Wahadzabe, Wadatoga, Wairaq na Wamasai walipata nafasi ya kuonesha ngoma zao za asili, vyakula, mavazi na mapambo ya kitamaduni.
Wageni na Wazawa walivutiwa na ngoma za asili ambazo ziliwakumbusha historia yao ya zamani ya mababu zao namna ya kuishi, kutumia dawa za kienyeji, vyakula asili na vifaa walivyotumia katika shughuli zao za kazi.
Mheshimiwa Theresia Mahongo amewashukuru wadau wa utalii wajasirimali, wageni na wananchi kwa kufanikisha tamasha hilo. Katika hotuba yake ya shukurani amesema tamasha la urithi limetukumbusha kudhamini utamaduni wetu. Tamasha hili litakuwa likifanyika kila mwaka mwezi wa tisa.
Mheshimiwa Theresia amesema nilikuwa naangalia ngoma ya asili ya wadatoga, mama mmoja akaniambia hao vijana unaowaona wa kiume hawawezi kucheza ngoma mpaka awe ameuwa mnyama. Ndipo anaruhusiwa kucheza na mkuki, tunawaita wapiganaji, Mheshimiwa Theresia akasema vijana wa sasa sijui kama wanafahamu kuhusu haya.
Mheshimiwa Theresia akasema nimepata wasaha wa kualikwa kwenye chakula cha mchana na wadatoga kama mlivyoona tumekula kwa pamoja. Ni familia ngapi wanakula na watoto wao ? tumesahau desturi ya kula pamoja.
Mheshimiwa Theresia amesema kama mlivyoona pombe ya kienyeji ya Wadatoga walianza kuwapa wakina baba na baadae wakina mama wakafuata. Hizo ndio namna zetu za kuishi zamani. Sasa huu ulimwengu wa kuishi na kununulia watoto wetu simu za kukwaruza ndio zinazosababisha mmonyoko wa maadili.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa