Na Tegemeo Kastus
Utoaji wa huduma kwa wateja lazima uimarike hasa kwenye huduma za dharura ambazo zinahitaji utatuzi wa haraka. Ili kujenga imani kwa wananchi kwamba mnajali na kusikiliza shida zao kwa wakati hasa wakati changamoto zinapojitokeza. Tujiwekee utaratibu mzuri wa kutoa taarifa kwa wananchi hasa zinazohusu marekebisho ya umeme ili kuwe na uelewa wa pamoja katika kutoa huduma.
Tukijenga mawasiliano mazuri kati ya shirika la umeme na wateja itahamasisha watu wengi kujitokeza kupata huduma. Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Abbas Kayanda alipokuwa akizungumza na wafanyakazi wa shirika la umeme Tanesco Karatu. Amesema shirika la umeme linafanya kazi nzuri sana hasa kipindi hiki cha masika chenye changamoto nyingi ya miundo mbinu ya umeme kupata hitilafu. Lakini pia changamoto ya matope kwenye barabara ili kufikia sehemu zenye shida imekuwa ikiathiri utendaji kazi.
Mh. Abbas Kayanda akiwa na meneja wa Tanesco Karatu baada ya kikao kifupi na wafanyakazi wa shirika hilo.
Mh. Kayanda amesema katika kuimarisha mawasiliano watendaji wa shirika la umeme lazima wakubali mabadiliko na waongeze kasi ya kufanya matengenezo pindi taarifa za hitilafu ya miundo mbinu zinapotolewa. Kuna changamoto za nyaya kukatika au nguzo kuanguka, shida zinazoweza kusababisha hatari ya kupoteza maisha kwa mwanadamu. Taarifa kama hizi zikitolewa na wananchi watendaji wa Tanesco msijivute kushughulikia, kwa sababu inatoa picha mbaya kwa wananchi. Dhamira yetu ijikite katika kutatua kero, ameongeza kusema nafahamu watumishi wa shirika la umeme Tanesco ni wachache lakini tujigawe kwa uchache wetu ili wananchi wapate huduma.
Mh. Kayanda amesema kumekuwa na malalamiko mengi kwa wananchi juu ya utendaji kazi wa shirika la umeme hasa katika utoaji wa huduma. Malalamiko hayo hayaleti afya katika kuendesha shirika, na badala yake yanajenga taswira mbaya. Amemuelekeza meneja wa shirika la umeme Karatu; kuja na mkakati madhubuti, utakaowezesha njia bora za kutatua kero za wananchi kwa wakati. kwa kuanza kuainisha mafundi wa umeme ambao, kama mwananchi anataka huduma ya kusuka waya katika nyumba yake wanaweza kufanya kazi kwa weledi wa taaluma.
Mh. Kayanda ameongeza kusema kuwe na uwazi ili kama mteja au mwananchi anahitaji kumuona meneja wa Tanesco aweze kumpata. Badala ya utaratibu wa sasa ambao mwananchi akitaka kumuona meneja anazungushwa bila ya kuwa na sababu za msingi. Tukiboresha utoaji wa huduma shirika litaongeza wateja wapya wengi wanaohitaji kuunganishwa na huduma ya umeme. Kwasababu wananchi watafahamu hatua za kufuata ili kuunganishwa na huduma ya nishati ya umeme. Amesema kuacha wananchi hewani bila kuwaeleza mahitaji yanayohitajika kwa mteja ili aweze kuunganishwa na umeme kunasababisha wananchi kuona wanapuuzwa tujifunze customer care.
wafanyakazi wa shirika la tanesco wakiwa katika kikao wa mkuu wa wilaya ya karatu ambaye hayupo pichani
Naye Meneja wa umeme wilaya ya Karatu Mhandisi Wilhelm Chami amemshukuru mkuu wa wilaya ya Karatu kwa kutembelea na kujionea utendaji kazi wa shirika hilo. Ameahidi kufanya mageuzi makubwa ya kiutendaji kwa kuhakikisha wanajenga mazingira ya uwazi katika utendaji wa kazi. Katika taarifa yake amesema shirika la umeme Karatu linasema kuna idadi ya watu zaidi ya 3000 wanaojiunga kupata huduma ya umeme kwa mwaka na kwa sasa kuna waatu zaidi ya 15000 ambao tayari wameshaunganishwa na umeme ukilinganisha na wilaya nyingine.
Katika unganisha umeme vijijini (Umeme wa Rea) Mhandisi Ndg Chami amesema kuna kampuni mpya ya Etdco ambayo ni kampuni tanzu ya Tanesco imepewa kazi ya kusambaza umeme vijijni. Kwa sasa Project manager wa kampuni amesha ripoti na ameenda Dar es salamu kukusanya vifaa kwa ajili kuanza kufanya kazi ya kusambaza umeme vijijni.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa