Mkuu wa wilaya ya Karatu Mhe. Theresia Mahongo amefanya mkutano wa hadhara katika kitongoji cha Ayalabe Magharibi katika kata ya Ganako. Mkuu wa wilaya ametembelea eneo la shule linalodaiwa kuvamiwa na kuleta mvutano kati ya shule ya Sekondari Ganako na mkazi anayelalamikiwa kujiongezea mipaka ya umiliki wa eneo la ardhi.
Mhe Theresia Mahongo katika mkutano wake wa hadhara alipokuwa akiwahutubia wananchi amewaelekeza watendaji wa ardhi wa wilaya ya Karatu kupima eneo la hekta 2.36 ili kubaini eneo na Mipaka halali ya ndugu Daniel Tewa. Mhe. Theresia ametoa maelekezo kwa ndugu Daniel Tewa kutoingilia eneo ambalo lipo nje ya heka 2.36 ambalo lilikuwa limelimwa na kuzuwa hofu kwa wananchi wanaotegemea miundo mbinu ya mabomba ya maji iliyojengwa nje ya umiliki wa eneo la ndugu Daniel Tewa.
Mhe. Mahongo amemuelekeza OCD wa wilaya ya karatu Musa Gumbo kumkamata na kumshitaki Ndugu Daniel Tewa. Mhe. Mahongo amesema vitendo vya kusambaza vinyesi; kelele za redio, vinavyolalamikiwa na wanafunzi wa sekondari ya Ganako si vizuri. Mhe. Mahongo amewahakikishia wanafunzi Ganako kwamba eneo lao la uwanja wa michezo litarudishwa.
Bango likiwa limebebwa na mwanafunzi wa shule ya sekondari Ganako likionesha madhila wanayokabiliana nayo.
Mhe. Mahongo amesema kulikuwa kuna vitisho kwenye eneo hilo hasa kwa wananchi kutishiwa na kunyimwa huduma za maji ambazo miundo mbinu yake imejengwa katika eneo linalodaiwa kuvamiwa na ndugu Daniel Tewa. Mhe. Mahongo amesema kuanzia leo watu wapate huduma za maji kama kawaida, amehimiza wananchi kutokuwa na wasiwasi.
Mhe. Mahongo amesema mzee Tewa alishinda kesi, juu ya umiliki wa eneo la heka 2.36 amesema serikali imeanza kufanya tathimini ya eneo hilo ili alipwe fidia. Mhe. Mahongo amesema baada ya kushinda kesi Mzee Tewa alipewa eneo la fidia na Halmashauri lakini akalikataa. Amesema sasa tunafanya tathimini na hatua za utathimini wa eneo hilo zikimalizika atapewa fedha zake ili eneo hilo litwaliwe kwa maslahi ya umma. Mhe. Mahongo amesema sheria za ardhi zinaruhusu utathimini kufanywa na mtendaji pamoja na viongozi wa mtaa endapo mhusika atakataa kufanya zoezi la utahimini wa ardhi. Mtendaji na viongozi wa mtaa watashirikiana watendaji wa ardhi kufanya utathimini eneo husika. Mhe. Mahongo amekemea watendaji wa ardhi wa wilaya kwa kushindwa kushauri kwa wakati namna ya kukabiliana na mgogoro wa eneo hilo amesema hatawavumilia, amewaonya kuacha kutingisha kiberiti. Mhe. Mahongo ameelekeza Mkurugenzi na Maafisa ardhi kuingiza kwenye bajeti ya serikali ya mwaka ujao wa fedha kiasi ambacho mzee Tewa anapaswa kufidiwa.
Bango likiwa limebebwa na mwanafunzi wa shule ya sekondari Ganako likioneshwa changamoto wanazokabiliana nazo.
Mhe. Mahongo amewaomba wananchi kuwa watulivu na wasijihusishe na vitendo vya uvunjifu wa amani. Mhe. Mahongo amesema hatua alizochukua, hajavunja sheria amefanya hayo kulinda amani ya Ganako sekondari, amani ya kata ya Ganako na amani ya Karatu. Mhe. Mahongo ameomba wananchi kutofanya malumbano ya aina yeyote, amesema hatavumilia mtu yeyote anayetaka kuvunja amani katika wilaya ya Karatu.
Bango likiwa limebebwa na mwanafunzi wa shule ya sekondari Ganako.
Afisa ardhi wa Wilaya Ndugu Lukasi Mfumbi amewambia wananchi kwamba wataalamu wa ardhi walikwenda kufanya tathimini ya hekari 2.36 wakiwa wameambatana na watendaji wa kata na viongozi wa mtaa. Afisa ardhi ndugu Mfumbi amesema ndugu Daniel Tewa alipewa taarifa ili ashiriki katika zoezi la utathmini wa eneo lake lakini alikataa. Amesema utathimini wa eneo hilo ulifanyika kwa kutumia sheria tatu ya kwanza ni; land acquisition act no. 47 ya mwaka 1997, sheria ya pili iliyotumika kufanya utathimini ni sheria no. 4, na 5 ya mwaka 1999 na kanuni zake za mwaka 2001. Sheria ya utathimini no 3 sheria ya utathimini no. 10 ya mwaka 2016. Amesema zote kwa pamoja zimetumika kufanya utathimini wa eneo ambalo anatakiwa apimiwe ili aweze kufidiwa. Ndugu Mfumbi amesema mhusika alifahamishwa kwa barua na ikitokea mhusika amekataa !! utathimini unafanyika kwa kupitia viongozi wa maeneo husika, viongozi wa mitaa na viongozi wa kata, amesema yote hayo yamezingatiwa. Ndugu Mfumbi amesema zoezi la utathimini linakaribia kukamilika baada ya kufuata hatua zote alizobainisha kupitia vifungu vya sheria ya ardhi alivyovitumia.
Katika mkutano huo wanafunzi wa shule ya sekondari walibeba mapango yao ambayo walisoma mbele ya mkuu wa wilaya ya Karatu. Mwanafunzi Athumani Katimba akisoma mabango hayo alisema wamechoshwa kuwekewa kinyesi mbele ya madarasa, na kusema wamechoshwa na magonjwa. Bango jingine alilosoma mwanafunzi Athumani lilisema tumechoshwa kelele za redio madarasani; na bango jingine lilisoma tunataka kucheza mpira ili tuinue vipaji vyetu, bango lingine likisoma tunataka tucheze mpira kwa amani tumechoka kuonewa, na bango lingine likisema tunaomba serikali itusaidie kuondoa uonevu na dhuluma zinazofanyika.
Bango likiwa limebebwa na mwanafunzi wa shule ya sekondari Ganako wakiomba kurudishiwa eneo lao la michezo.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa