Na Tegemeo Kastus
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Karatu ndugu Waziri Mourice, pamoja na timu ya uendeshaji wa Halmashauri wamefanya ziara ya kutembelea miradi ya ujenzi inayoendelea katika Tarafa ya Karatu.
Lengo la ziara hiyo ni kupata uelewa wa pamoja na kushauri juu ya hatua mbalimbali za miradi ili iweze kukamilika kwa wakati. Ndugu Waziri Mourice amesema lengo la Halmashauri ni kukamilisha mapema na kwa wakati majengo matatu ya hospitali ya wilaya ambayo ni jengo la utawala, jengo la wagonjwa wa nje na jengo la maabara.
Ndg. Mourice amesema wamenunua mbao kutoka Iringa zenye ukubwa wa cubic meter 40 ambazo zimesaidia kupiga draft darini jengo la wagonjwa wa nje na kusaidia kupaua maabara na kupiga draft jengo la utawala. Ndg. Mourice amesema wamenunua siment kutoka Tanga siment Tanga ambayo inasaidia kupiga ripu majengo, amesema vitu vyote vienye uhitaji wa kununua kiwandan vitanunuliwa kiwandani ili kupunguza gharama za ujenzi, amesema kwa sasa hakuna kitu kitakachonunuliwa Karatu. Gharama ya simenti mfuko mmoja kutoka kiwandani mpaka eneo la mradi ni Tsh. 14750 na Karatu mfuko mmoja wa simenti unauzwa 17000, amesema mbao cubic meter 40 kutoka mafinga zimegharimu Tsh. 23,000,000 ambazo zimetumika kwa majengo yote matatu wakati walishawahi kupaua jengo moja kwa gharama Tsh. 25,000,000 kwa mbao zilizotoka Karatu.
Timu ya uongozi wa Halmashauri ikiwa katika picha ya pamoja eneo la ujenzi wa hospitali ya wilaya
Ndugu Mourice amesema ujenzi wa bweni karatu sekondari unaendelea vizuri, kwa sasa ujenzi uko katika hatua ya ujenzi wa Msingi. Bweni hilo linajengwa baada ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo kutoa kiasi cha shilingi million 70 kusaidia ujenzi wa bweni hilo linalokadiriwa kuchukua wastani wa wanafunzi 85 kwa mwananfunzi mmoja mmoja bila kuweka vitanda vya juu na chini. Mpaka sasa tripu 20, za mawe zimepelekwa eneo la ujenzi na tofali 1200 kwa ajili ya kujenga msingi kwa kulaza matofali na mifuko 300 imeshapelekwa eneo la ujenzi.
Jengo la two in one linalojengwa na TASSAF katika Kituo cha Afya Karatu linalogharimu million 66, mradi unaeendelea vizuri umefika 78%. Amesema jengo la wodi ya mama na mtoto linaloendelea kujengwa liko katika bajeti ya mwaka huu na limetengewa million 35, amesema wanafikiria kuwanunulia vifaa moja kwa moja kituo hicho cha afya ili kituo chenyewe kijikite katika ujenzi. Ndugu Mourice amemuelekeza daktari kiongozi wa kituo cha afya Karatu kumwaga Moram ili kufukia mashimo yaliyo izunguka hospitali lakini pia kukabiliana na hali ya tope iliyopo katika eneo hilo.
Ndugu Mourice amesema katika mradi wa soko wanataka waingie mkataba na mafundi katika ujenzi wa vizimba wakubaliane malipo kwa tofali. Amesema jumatano asubuhi timu ya uongozi wa Halmashauri itakwenda kusimamia setting ya ujenzi wa vizimba.
Ndugu Peter Ngumuo kwa niaba ya wajumbe wa timu ya uendeshaji ya Halmashauri amepongeza miradi, amesema wamefurahi kutembelea miradi hiyo na kupata maelezo ya kina ya hatua za ujenzi zilipofikia jambo ambalo limewapa uelewa mkubwa.
Timu ya uongozi wa halmashauri ikiwa katika eneo la ujenzi wa bweni sekondari ya wavulana karatu
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa