• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Complains |
Karatu District Council
Karatu District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dhamira na Dira
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
    • Vitengo
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
  • Madiwani
  • Miradi
    • TASAF
    • BOOST
  • Machapisho
    • Hali ya Uwekezaji
      • Business License Form
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Habari
    • Hotuba kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha

TUCHUKUE TAHADHARI, UGONJWA WA MNYAUKO WA MAHINDI

Posted on: April 10th, 2021

Na Tegemeo Kastus

Wakulima waaswa kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa mnyauko wa mahindi ulioanza kuathiri eneo la Bonde la Eyasi. Ugonjwa huo wenye tabia ya kudumaza mahindi na kusababisha mnyauko  unasambaa kwa njia ya maji, mvua, upepo vifaa vya kilimo ambavyo vimetumiwa katikashamba liloathirika na kwenda kutumika sehemu nyingine  bila kusafishwa vizuri.

Tatizo hilo limebainika katika ziara ya mkuu wa wilaya ya karatu Mh. Abbas Kayanda pamoja na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama walipotembelea shamba la  taasisi ya Magereza ambalo kiasi cha hekari kumi na tano zimeharibika kutokana na kuathiriwa na ugonjwa wa mnyauko wa mahindi MLND (Maize lethal necrotic diseases). shamba lililotembelewa  walipanda mahindi kwa kutumia mbegu aina ya m seed co 513 na  mahindi hayo yaliyopandwa kuanzia mwezi wa kumi yameathirika sana na ugonjwa wa mnyauko wa mahindi ukilinganisha na mahindi ambayo yalipandwa kabla mvua kuanza kunyesha.

Mh. Abbas Kayanda akiangalia  shamba la taasisi ya magereza lililoathiriwa na ugonjwa wa mnyauko wa mahindi

Mh. Kayanda amehimza elimu kutolewa kwa wananchi katika mikutano ya hadhara ya kijiji na ngazi ya kitongoji, ili kuwaelimisha wananchi juu ya ugonjwa wa mnyauko wa mahindi. Amesema wananchi wakijengewa uelewa inakuwa ni rahisi kukabiliana na ugonjwa huo, kwa sababu watalima kwa kufuata maelekezo ya maafisa kilimo.

Mh. Kayanda amemuelekeza Afisa kilimo wa wilaya kuandaa kikao cha wadau wa kilimo kitakachohusisha Mawakala wa mbegu za kilimo na pembejeo, wakulima na wataalamu wa kilimo ili kujadiliana na kuja na mapendekezo yatakayosaidia serikali kukabiliana na changamoto ya ugonjwa wa mnyauko wa mahindi shambani.

Afisa kilimo wa kata ya Baray Ndg. Johnson Christian Ishengoma amesema ili kukabiliana changamoto ya mnyauko wa mahindi, wakulima wanapaswa kuwahi kupanda mazao ardhini katika kipindi cha mwezi tisa au kabla kwa sababu virusi wanaosababisha mnyauko wa mahindi wanakuwa dhaifu na wamefubaa hivyo hawawezi kushambulia mmea wa mahindi. Ameongeza kusema katika kipindi cha kupanda mkulima anapaswa kupuliza dawa ya kuuwa wadudu kama utitiri na kimamba ili kuwezesha kukinga mmea na wadudu wanaoathiri mimea ya mahindi.

Mh. Abbas akivuka korongo kuelekea eneo la mashamba katika kata ya Baray

Ndg. Ishengoma amesema mahindi yanayopandwa wakati mvua zimeshaanza kunyesha, yanaathirika sana na ugonjwa wa mnyauko wa mahindi kwa sababu virusi vinakuwa vinafanya kazi (active) na mkulima hugundua mmea umeathirika wakati mhindi unapokuwa katika kimo cha kwenye magoti hivyo inakuwa ni vigumu sana kukabiliana na athari za kirusi huyo kwa sababu mpaka sasa hakuna dawa ya kuwauwa.

Ndg. Ishengoma amesema njia nyingine ni kushauri wakulima kupumzisha shamba kwa kupanda mazao mengine kwa muda wa miaka mitatu ili virusi vidhoofu na vipoteze uhai ardhini. Amesema hiyo inasaidia kulipa shamba rutuba lakini inaondoa virusi hao wanaokausha mahindi kwa sababu hawana uwezo wa kuathiri mazao mengine.

Ndg. Ishengoma amesema shamba lililoathiriwa na virusi vya ugonjwa wa mnyauko mahindi mabua yake yanapaswa kuchomwa na kuteketezwa. Hayafai kulisha mifugo wa sababu yanasababisha kansa kwa wanyama, amesema hata mnyama atakayechinjwa aliyekuwa akitumia mabuaa mahindi yaliyoathirika kwa kunyauka yanaathari za moja kwa moja kwa binadamu. Amesema tunahitaji kuchukua tahadhari juu ya ugonjwa huu, hata kwenye vifaa au nguo ambazo mkulima atafanya nazo shughuli za kuteketeza mahindi yaliyoathirika kwa ugonjwa huu lazima asafishe kwa maji na sabuni ili asisambaze vimelea hivyo kwenye shamba jingine.

Mh. Abbas Kayanda akitembelea eneo la Mashamba katika kata ya Baray


Matangazo

  • Matokeo ya upimaji wa Kitaifa kidoto cha pili January 07, 2024
  • Halmashauri ya Wilaya ya Karatu Uchaguzi wa Wanafunzi wa kidato cha kwanza, 2024 December 18, 2023
  • Matokeo ya Darasa la Nne January 07, 2024
  • NAFASI ZA KAZI 2024 April 21, 2024
  • Angalia Zote

Taarifa Mpya

  • MADAKTARI BINGWA WA SAMIA AWAMU YA TATU WATUA KARAU

    May 12, 2025
  • KARATU WASAPOTIJUHUDI ZA RAIS SAMIA WATANGAZA UTALII WA NDANI

    May 11, 2025
  • MILIONI 400 ZATOLEWA KARATU, KUJENGA MABWENI NA MADARASA EYASI SEKONDARI

    January 30, 2025
  • WASIMAMIZI WAASWA KUSIMAMIA VIAPO VYAO KUELEKEA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024.

    November 23, 2024
  • Angalia Zote

Video

DC KOLIMBA ATATUA KERO TARAFA YA EYASI KARATU
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fursa za Uwekezaji

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Wizara ya Fedha na Mipango
  • Jamvi la Habari
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karatu District Council

    Sanduku la Posta: P.O Box 190

    Simu: +255 272970648

    Simu ya Mkononi: 0754773947

    Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa