Kasi ya magonjwa yanayoambukizwa kwa njia ya ngono isiyo salama imeongezeka duniani. Utafiti uliofanywa na shirika la afya WHO na baadae taarifa yake kutolewa na kituo cha televisheni cha CNN umesema karibu kila watu 25 mtu mmoja anadalili za magonjwa yanayosababisha na ngono isiyo salama.
Dkt. Mellanie Taylor aliyeongoza utafiti huo uliotolewa Alhamisi anasema watu wamekuwa wanajihusisha na mahusiano ya ngono hatarishi kiafya. Tabia zinazo sababisha magonjwa ya ngono (sexual trasnsmited disease Infection) STIs ambayo pia hufahamika kama STD’s. Dkt. Mellanie anasema magonjwa kama Kaswende Gonorea upungufu wa kinga mwilini ni miongoni mwa magonjwa ambayo husababishwa na kufanya ngono isiyo salama.
Dkt. Vicent Gyunda ni daktari kiongozi katika kituo cha afya Karatu. Dkt. Vicent anasema ni kweli ngono isiyo salama inasababisha magonjwa ya zinaa. Anasema kwa takwimu za Mwaka huu January mpaka March yaliripoitiwa matukio 1879 ndani ya wilaya ya Karatu kati ya hayo matukio 219 yaliripotiwa kituo cha afya Karatu.
Dkt Vicent Gyunda
Dkt. Vicent anasema magonjwa hayo yamegawanyika kwa makundi; yapo magonjwa yanatokana na Genital discharge syndrome, ambayo ni mlundikano wa magonjwa kama Gonorea. Kuna kundi la magonjwa yanayotokana na Genital ulcer diseases, ambayo inakuwa kama mchubuko au kidonda kisichokuwa na maumivu yeyote sehemu za siri. Hii hujitokeza kwa mtu mwenye magonjwa kama kaswende. Kuna magonjwa yanahusu jinsia ya kike katika kundi hili kuna Pervic inflammatory disease. Hii huhusisha viungo vyenye mahusiano na tendo la ngono ambayo husababisha viungo vya uzazi; kama nyumba ya uzazi, shingo ya kizazi , nyonga kupata maambukizi haya yanayofuata mfumo huu wa viungo vya uzazi ambavyo huaathirika kwa pamoja na hutokea hasa kwa wanawake. Dalili zake ni mauvimu chini ya tumbo, ambayo pia husababisha badiliko asili la umbo kama kuwa na wekundu na kuondoa muonekano wa kawaida.
Dkt. Vicent anasema visababishi vya magonjwa haya ni mazingira hatarishi. Dkt vicent anasema kuwa na mahusiano na mtu zaidi ya mmoja ni chanzo kwa sababu cha watu kufanya ngono hatarishi ambayo muathirika anapata kwa kushindwa kutumia kinga. Dkt vicent anasema hali ya umasikini husababisha baadhi ya watu kujiingiza katika ngono hatarishi kutokana na uduni wa kipato.
Dkt. Vicent anasema upo pia uwezekano wa mama mjamzito kumuambukiza mtoto mchanga haya magonjwa wakati wa kujifungua, kutokana na michimbuko au msuguano wakati wa kujifungua. Dkt vicent anasema kuna swala la mila potofu, ambazo husababisha kuzidi kuenea kwa magonjwa yatokanayo na ngono zembe. Imani za kuridhishana wajane au kufanya ngono na mtu wa rika flani ili ufanikiwe kupata fedha.
Dkt Vicent anasema kuna visababishi ambavyo ni kama wakala wa kusambaza maradhi, mathalani virusi ambavyo huleta magonjwa kama Upungufu wa kinga mwilini. Kuna bacteria ambao husambaza magonjwa yanayotokana na ngono zembe. Lakini kuna protozoa ambao husambaza magonjwa yanayotokana na ngono zembe.
Dkt. Vicent anasema namna kuepuka madhara ya magonjwa yanayosababishwa na ngono zembe ni kuacha kufanya ngono zembe kwa kujizuia tamaa za mwili. Dkt. Vicent anasema tunashauri kama mtu hawezi kujizuia tama za mwili, kutumia mpira ambao utamkinga na magonjwa hatari yanayotokana na ngono zembe. Dkt vicent anasema njia nyingine sahihi ni kuwahi kupata tiba mtu aliyeathirika ambayo husaidia kupunguza maumbukizi mapya. Dkt vicent anasema wao kama idara ya afya hujikita kutoa elimu kwa wananchi kupitia kliniki za mkoba.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa