Madiwani wa wilaya ya Karatu pamoja na watendaji mbalimbali wa Halmashauri wametembelea leo shule ya OLdean seondari, shule ya Msingi Gyetighi na Kituo cha watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu. Ziara ililenga kuona shughuli zinazofanywa na shirika la Rift Valley Children Fund ambalo linashirikiana na serikali kuimarisha miundo mbinu ya elimu.
Mkurugenzi wa Rifty Valley Ndugu Mmassy amesema katika kipindi cha miaka 15 wametoa vijana waliohitimu elimu ya juu 79 katika fani mbalimbali na kuajiriwa. Amesema pamoja na mafanikio hayo shirika limeendelea kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu bora. Shirika limejenga Maktaba pamoja na Kuweka vitabu, Maabara na vifaa vyake, Jengo la utawala, Madarasa, pamoja na nyumba za walimu.
Ndugu Mmassy amesema wao wanajihusisha pia na kulea watoto wanao toka katika mazingira magumu na yatima. Shirika limeajiri wakinamama zaidi 130 kwa ajili ya kulea watoto kwenye kituo chao. Ndugu Mmasy amesema wanatoa huduma za afya kwa wananchi wa Oldean na kutoa rufaa pia kwenda Hospitali ya Fame na Selian Jijini Arusha. Wanatoa pia mikopo kwa wananchi wa eneo la Oldean ili kuwainua kiuchumi.
Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari Oldean ndugu Yuda John ambaye shule yake ilitembelewa, amesema shule ina walimu 15 wenye ajira ya kudumu na walimu wa muda 11. Shirika linasaidia watoto 46 ambao ni watoto yatima na kusaidia kulipa mishahara ya walimu wa muda. Mwalimu Yuda amesema shirika la Rifty Valley Children Fund, linampango wa kujenga mabweni kwa ajili ya wanafunzi wanaotoka mbali na yatachukua wanafunzi 480.
Mwalimu Yuda amesema lengo ni kuongeza uwezo wa kuchukua wanafunzi zaidi kama ilani ya chama cha mapinduzi inayosimamiwa na serikali ya awamu ya tano inavyoelekeza. Elimu ya msingi na sekondari mpaka kidato cha nne ni bure, ili kuruhusu watoto wanaokabiliwa na changamoto mbalimbali kupata elimu. Amesema changamoto inayowakabili kwa sasa ni upatikanaji wa nishati ya umeme, amemuomba katibu Tarafa wa tarafa wa Karatu kuwasaidia kupata umeme kupitia mpango wa REA.
Madiwani pia walipata nafasi ya kutembelea shule ya msingi Gyetighi ambayo inasimamiwa na serikali ikishirikiana na Rift Valley Children Fund. Mwalimu mkuu ndugu Fidelis,Anthony amesema shule ina walimu 8 wa kuajiriwa na serikali na walimu 16 wa muda na walimu wanafunzi 5. Mwalimu Fidelis amesema shirika linatoa chai kwa walimu asubuhi na uji kwa wanafunzi, chakula cha mchana kwa wanafunzi na walimu pamoja na kutoa huduma ya afya.
Shirika linatoa elimu ya malezi kwa walimu hasa ukizingatia kwamba shule yao ni ya mfano, mwanafunzi hachapwi bali anapewa adhabu ndogondogo kama kupiga magoti, kuruka kichura chura na kushauriwa. Shirika limejenga viwanja vya michezo pamoja na kutoa vifaa vya michezo na kuweka uzio na mageti. Shirika linatoa motisha kwa walimu ili kuwapa ari ya kufanya vizuri katika ufundishaji..
Mweneyekiti wa Halmashauri Mhe. Jublate Mnyenye ameshukuru kwa namna ambavyo Shirika linavyofanya kazi kwa niaba ya serikali. Ameomba watumishi wafanye kazi pamoja na shirika hilo na kutoa ushirikiano. Amesema madarasa hayawezi kufaulisha wala maabara peke yake; kwa kuwaachia majukumu walimu peke yao, wazazi timizeni wajibu wa kuwasimamia watoto ili wafaulu vizuri. Mhe. Jublate amesema kama kunajambo linaleta kikwazo katika maswala ya utendaji, litolewe taarifa sehemu husika hatua kwa hatua. Amesema tukipuuzia jambo likawa kubwa likaenda ngazi za juu bila kufuata hatua litaonekana kuna Personal interest.
Mhe. sabina na wataalamu wakiangalia kwa tumiaa kifaa maalumu kuangalia sampuli ya jani katika maabara ya bailojia
Waheshimiwa madiwani wakisikiliza kwa makini maelekezo ya mkuu wa shule Ndugu Yuda John kwenye maabara ya Kemia
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa