Zoezi la kupanda miti wilaya ya Karatu limefanyika katika kijiji cha Rhotia kati katika Mlima moyo. Mkuu wa wilaya ya karatu Mhe. Theresia Mahongo aliongoza zoezi la kupanda miti, na ameshukuru wadau kwa kujiotokeza kusaidia zoezi la kupanda miti.
Mhe. Theresia Mahongo amesema lengo ni kufanya Karatu kuwa ya kijani tena. Ametoa wito kwa wananchi kuitunza miti ili ikue, awali miti 1000 ilipandwa na sasa tumepanda miti 2500 na kufanya idadi ya miti iliyopandwa kipindi hiki kufika 3500. Mhe. Theresia amesema awali zoezi la kupanda miti lilitakiwa lifanyike tarehe moja mwezi wanne lakini kutokana na sababu za mabadiliko ya hali ya hewa zoezi limefanyika mwezi wa tano. Amesema Mlima moyo umekuwa ukisaidia Rhotia kupata mvua nyingi, ni vyema tukaendelea kutunza mazingira ili mazingira nayo yatutunze.
Mhe. Thereseia ameelekeza uongozi wa kijiji cha Rhotia Kati kutunza miti iliyopandwa. Amesema ni vyema kukawa na utaratibu mzuri wa kuvuna misitu kwa kuhakikisha pindi wanapokata miti kuwe na utaratibu wa kupanda miti mingine. Mhe. Theresia ameuhimiza uongozi wa kijiji kuhakikisha miti haikatwi hovyo lakini pia kusimamia na kuilinda miti iliyopanda. Amesema Mlima moyo usingekuwa kama ulivyo endapo eneo hilo la mlima lisingekuwa lianatunza.
Mhe .Theresia ametoa cheti kwa Mwenyekiti wa kijiji cha Rhotia kati Ndugu Andrea Mallu na wananchi wake kwa juhudi zao nzuri za kutunza mazingira. Amesema serikali inatambua mchango wa wananchi wa kijiji cha Rhotia kati katika utunzaji wa mazingira. Kijiji hicho cha Rhotia kati, kimepanda miti zaidi ya hekari 100. Mhe. Theresia ametoa cheti cha kuwatambua Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongo na ametoa cheti pia kwa club ya mazingira. Amewapongeza mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro kwa kutoa miche ya miti iliyopandwa Mlima moyo na shule mbalimbali za kata ya Rhotia na zahanati.
Naye muwakilishi wa mamlaka ya Ngorongoro ndugu Peter Duwe ameomba wananchi kuilinda miti hiyo iliyopandwa. Ndugu peter amesema gharama ya kuitunza miche hiyo ni kubwa haipendezi kuona miche hiyo inashindwa kustawi vizuri. Ameshukuru kwa uongozi wa kijiji kwa kuendelea kutunza miti vizuri iliyopandwa awali. Ndugu Duwe amesema miti hiyo licha ya kutolewa na mamlaka ya Ngorongoro bure ili ipandwe, isipostawi ni hasara. Amesema maadui wakubwa wa misitu ni wanyama wanaofugwa nyumbani na shughuli za binadmu ambazo kwa pamoja zinachangia kuharibu miti. Ndugu peter amehimiza viongozi wa kijiji kutunza miti hiyo iliyotolewa na mamlaka ya hifadhi vyema.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa