Na Tegemeo Kastus
Miti milioni moja na nusu inatarajiwa kupandwa katika wilaya ya Karatu, miti hiyo itapandwa katika taasisi za serikali na watu binafsi lengo likiwa ni kufanya wilaya ya Karatu kuwa ya kijani. Wito umetolewa kwa wananchi kushiriki katika zoezi la upandaji wa miti kwa kuhakikisha kila familia inapanda miti kumi katika eneo inaloishi.
Hayo yamesemwa na Katibu tawala wa wilaya ya Karatu Bi. Faraja Msigwa alipoongozwa wananchi na watendaji wa serikali katika siku ya kupanda miti akimuwakilisha Mkuu wa wilaya ya Karatu. Zoezi la upandaji wa miti limefanyika katika eneo inapojengwa hospitali ya wilaya ya Karatu katika kijiji cha changarawe. Amesema lazima tupande miti ili kuzuia mmonyoko wa udongo unaosababishwa na ardhi kuwa wazi. Amesema kupanda miti kuna faida kubwa, kwanza inasaidia kutunza na kuweka hali ya hewa vizuri na kupata miti ya kivuli inayosaidia kupata maeneo ya kupumzika.
Wananchi wakishiki zoezi la upandaji miti katika Hospital ya wilaya ya Karatu.
Bi, Msigwa amesema zoezi la kupanda miti ni zoezi endelevu tunahitaji kutunza vyanzo vyetu vya maji, ametoa rai kwa watendaji wa serikali kuhamasisha watu katika maeneo yao ya kiutendaji ili kuhakikisha mikakati iliyowekwa na wilaya inafikiwa. Bi Msigwa amepongeza na kushukuru wadau mbalimbali walioshirikiana na wilaya katika kuwezesha zoezi la kupanda miti linafanikiwa.
Afisa misitu wa wilaya Ndg. Regnald Hallu amesema wadau wamazingira wameweza kupanda miti akatika kijiji cha Ayalalio, Buger, kitongoji cha Ngorong’aida na maeneo ya taasisi kama Qaru sekondari, Oborshan sekondari, Endabash sekondari Endarofta sekondari, kitongoji cha bwawani na bado zoezi la usambazaji wa miche ya miti inaendelea.
Ndg. Hallu amesema taasisi ya Mviwata ya Arusha imeweza kuanzisha mradi wa vitalu vya miche ya miti katika vijiji vya Slahamo, Buger, Rhotia Kainam, Kambi ya simba na Upper kitete. Amesema jumla ya miti 15000 imepandwa katika msitu wa Kansay. Amessema taasisi ya Mviwata imefanikiwa kufikia vijiji 20 na kufanikiwa kupanda miti zaidi ya 63000.
Naye Makamu mwenyekiti wa Mviwata Bi. Anna Efata ametoa shukrani kwa Halmashauri Karatu kwa kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na Mviwata Arusha. Amesema sasa ni jukumu la wananchi kutunza na kuhifadhi miche ya miti iliyopandwa, haipendezi kuona watu wanafanya uharibifu katika maeneo ambayo miche ya miti imepandwa. Swala la kulinda na kuhifadhi miche ya miti ni jukumu letu sote.
Bi. Efata ameshukuru wadau wengine kama Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro, wadau wa IDP kupitia mradi wa kilimo endelevu , wadau wa shirika la World vision na Ganako youth foundation. Amesema maono ya Mviwata ni kuendelea kuhamasisha na kushauri wananchi watunze mazingira.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya ya Karatu Ndg. Ally Mdangaya akipanda mti wakati wa zoezi la upandaji wa miti.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa