NA TEGEMEO KASTUS
Shamba darasa la vitunguu la White onion na shamba la darasa la vitunguu red Bombay ni moja ya vitu viliyokatika banda la nane karatu. Vitunguu ni zao kuu la biashara katika tarafa ya Eyasi na nizao linalochangia karibia 29% ya mapato ya ndani wilayani Karatu.
Kitunguu cha white Onion kinapendwa sana na watu wa wanaofanya biashara za hotel, na kitunguu cha Red Bombay (HYBRID) ni ktunguu kinachozaa sana na ni aina ya mbegu inayotumiwa na wakulima karatu. Hayo yamesema na Afisa Kilimo Jonhson Ishengoma, ambaye amesema kwenye shamba darasa hilo kuna kabichi kitaalami inaitwa Imani F1 ambayo inatabia ya kuzaa kwa wingi matunda makubwa na inalimwa maeneo ya midabini Karatu.
Maonyesho ya sherehe za nane nane kanda ya kasikazini yanafanyika katika viwanja vya nanenane mkoa wa Arusha. Wilaya ya Karatu ni moja ya wilaya ambazo zimeshiriki katika maonesho ya nane Arusha. Ndg. Ishengoma anasema katika shamba darasa kuna hoho chotara ambayo inazaa sanaa na inatoa matunda makubwa. Katika banda la Karatu, kuna shamba darasa la Bilinganya ambayo mbegu zake ni chotara na inazaa sanaa. Zaidi katika shamba darasa wataalamu wa kilimo wanatoa ujuzi wa kutumia eneo dogo la ardhi kufanya uzalishaji mkubwa na wenye tija kwa kufuata kanuni bora na za kisasa za kilimo.
Huu ni mmea unaitwa Betroot ambao tunda lake linatengeneza juice inayoongeza damu kwa wingi pamoja na kinga mwili
Kitalu cha Ngano katika shamba darasa la Halmashauri ya karatu na moja ya zao linalotolewa maelezo ya kitaalamu na wataalamu wa kilimo kuongeza uelewa wa kilimo cha zao hilo, inachukua siku tisini mpaka kukua, ngano hutumika katika kutengeneza mikate, na chapati. Kuna zao la maharage ambalo linapatikana katika shamba darasa la Halmashauri ya Karatu pamoja na hilo Kuna shamba darasa la mboga mboga la mnafu ambao unachukua siku thelathini kwa mkulima kuanza kuchuma, lakini pia kuna shamba darasa la karoti nantees. Katika shamba darasa kuna mboga mboga aina ya betroot lakini tunda lake likitengenezwa kama juice husaidia kuongeza kingamwili na damu, kuna nyanya ndefu (Anna F1) lakini pia kuna utaaalamu kulima bustani ya karatasi ya nylon ambayo imetengenezwa kitaaluma kuzia magugu lakini inamwagiliaji wake niwa kimkakati kwa njia ya mirija ya bomba za maji (dripping) uatapata kuona shamba la viazi lishe katika banda la Halmashauri ya Karatu. Sambamba na mazao hayo kuna shamba darasa la Ngwara zao linalostahimili ukame kwa mujibu wa Afisa kilimo Ndg. Ishengoma, lakini ni zao ambalo soko lake linakuwa kwa kasi sana siku za hivi karibuni, utaweza kuona shamba darasa la ndizi na kujua namna bora za ulimaji wa ndizi kitaalamu.
Mkulima wa kahawa ndg. Filipo Safari ambaye amepiga hatua katika kilimo kwa kuweza kuongeza thamani zao la kahawa anasema nane ni fursa kwao kama wakulima wadogo kutafuta masoko ya mazao wanayoyalima. Pamoja na hilo wanatumia fursa ya maonesho ya nane nane kujifunza mambo mengine yanayohusiana na kilimo kwa kuangali wakulima wa sehemu nyingine wanamambo gani ya ziada.
Ndg. Safari anasema alianza kilimo cha kahawa kupitia shamba ambalo mzazi wake alianza kulima kilimo hicho na yeye akaendeleza walipoishia wazazi wake. Anasema mpaka sasa analima shamba la heka tano, amesema wanaisindika na kuitengeneza kahawa wao wenyewe. Ndg. Safari anasema kahawa yao ni bora na yenye ladha tofauti na kahawa nyingine. Anasema kitu kinachachochangia kahawa hiyo kuwa tofauti na nyingine kwa sababau wanatumia mbolea zisizo na kemikali za viwanda katika kuzalisha kahawa na badala yake hutumia samadi inayatokana na wanayama wanaofugwa nyumbani.
Fransika Joseph mmoja ya wakulima wa viazi lishe anasema maonyesho ya nane nane ni muhimu kwao sana. Anasema kampuni ya Qwatema inajihusisha na kuongeza thamani katika mazao ya viazi lishe ambayo wanatengeneza bidhaa kama unga lishe, biskuti, clips na tambi zinazotengenezwa na viazi lishe. Kuongezan thamani ya zao kumemsaidia kutanua wigo wa uzalishaji wa zao hilo lakini umenufaisha zaidi watoto wadogo ambao hutegemea unga wa viazi lishe kwa sababu ya kuwa na virutubisho vingi vya kujenga mwili. Sambamba na hilo ungalishe unasaidia watu wenye changamoto za kutumia vyakula vienye sukari, amesema ukitumia vyakula ambavyo vinatenegenezwa na viazi lishe inasaidia watu kupata ladhaa ya sukari kutoka kwenye chakula chenyewe ambayo haina athari katika mwili.
Hizi ni hoho (hybrid)
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa