Zoezi la maboreho ya daftari la wapiga kura limeingia katika siku ya tatu ya uandikishaji wilayani Karatu. Jumla ya vituo 222 vya uandikishaji pamoja na Maafisa waandikishaji na BVR KIT Operators 444 wamesambazwa sehemu mbalimbali za wilaya ya Karatu.
Afisa wa tume ya Uchaguzi Bi, Nice Msigaro ambaye anatembelea vituo mbalimbali vya uandikishaji anasema muitikio siyo mubaya sana. Watu wameitikia vizuri amesema kama kituo cha Sokoni mjini na Bwawani Karatu watu zaidi ya 91 walijiandikisha jana na vituo vya kijijini vilikuwa na wastani wa waandikishaji wa watu 20 kwa siku.
Bi, Nice amesema kuna vituo vitakuwa na watu wengi sana siku za mapumziko ya wiki hasa vituo vyienye wafanyakazi katika mashamba makubwa, watatumia siku za mapumziko kujiandikisha au kuboresha taarifa zao kwenye daftari la Maboresho la wapiga kura. Amesema lengo la kusambaza vituo vingi ni kuwezesha kufikia watu katika maeneo yao, waweze kubadilisha taarifa zao kama wamehama maeneo waliokuwa wamejiandikisha awali. Lakini pia kuandikisha upya watu waliopoteza kadi zao za kupiga kura baada ya kupata barau ya utambulisho kutoka kwa balozi au taarifa ya kupoteza kitambulisho kutoka polisi. Watu wengine wanaopaswa kuandikishwa ni watu waliofikia umri wa miaka 18 au watu watakao fikia umri wa miaka 18 mwezi wa kumi mwakani.
Maafisa waandikishaji wakisaidia Mwananchi kuweka alama za vidole katika kituo cha sokoni Karatu
Bi, Nice amesema changamoto wanazopata kwa uandikishaji ni wakati mtu anapojiandikisha kutoka eneo moja, halafu anaenda kituo kingine kurekebisha taarifa zake. Bi.Nice amesema wamepata changamoto kama hiyo tarafa ya Mbulumbulu baada ya mwandikishaji kujiandikisha wilaya ya Monduli jana na anataka kuboreshewa taarifa zake katika wilaya ya Karatu. Haonekani kwenye data base ( kazi data) ya daftari la wapiga kura, kwa sababu taarifa bado hazija huishwa kwenye daftari la kudumu la wapiga kura. Amesema matukio kama hayo hulazimu mwandikishwaji huyo kurudia kujiandiksha upya na taarifa za awali kukatwa. Bi nice ametoa wito kwa wananchi wengine kujitokeza kujiandikisha kwenye maeneo yao wanayoishi badala ya kujiandikisha sehemu nyingine halafu wanakwenda kurekebisha kwenye eneo lao la makazi.
Naye Afisa Tehama ndugu Peter Panga anayejihusisha mfumo wa marekebisho wa mitambo ya uandikishaji wapiga kura, amesema wamejipanga vizuri kuondoa vikwazo vyovyote vitakavyotokeza wakati wa zoezi hilo. Amesema upo uwezekano wa waandikishwaji kuongezeka zaidi siku za mwisho kuliko idadi ya watu wanaojitokeza hivi sasa. Amesema hata hivyo hakuna tatizo kwa sababu waandikishaji kadri siku zinavyokwenda wanazidi kuimarika katika utendaji wa kazi na kasi inaoongezeka. Amesema awali kulikuwa na changamoto za vifaa vituo tofauti tofauti lakini changamoto hizo zimesimamiwa vizuri na Maafisa waandikishaji wa wilaya wanaozunguka vituo mbalimbali.
Ndugu Peter ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kujiandikisha mapema ili wasije kukosa haki yao ya msingi ya kupiga kura wakati wa uchaguzi. Amesema siku za mwisho zinaweza kuwa na msongamano wa watu wengi ambao wangeweza kujiandikisha wakati wa siku za kawaida. Zoezi la uandikishaji limebakiza siku nne kukamilika katika wilaya ya Karatu.
Ndugu Peter na Bi, Nice wakifanyia marekebisho Mashine ya BVR KIT baada ya kuleta dosari.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa