Kikao cha baraza la madiwani cha robo ya pili ya mwaka kimekaa siku ya kwanza, kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Karatu. Madiwani wa kata zote wamewasilisha taarifa za kata kwenye kikao cha baraza.
Katibu wa kikao cha baraza la Madiwani Ndugu Waziri Mourice amesema tangu serikali ya awamu ya tano imeingia kumekuwa na ongezeko la uandikishaji wa wanafunzi. Amesema kuna wanafunzi 4084 wa sekondari walioripotiwa kufaulu; lakini walioripoti shuleni mpaka sasa ni wanafunzi 3574, kuna wanafunzi 510 ambao hawajaripoti shuleni. Hawa wanafunzi wapo kati kata zetu, amesema wanafunzi ambao hawahudhurii shuleni kwa upande wa kata za Baray na Mang’ola huwa wanaenda kufanya kazi katika mashamba ya vitunguu.
Amesema uandikishaji wanafunzi wa awali ni 73% katika malengo ya uandikishaji wa 100%, uandikishaji wa wanafunzi wa darasa la kwanza ni 93 % kuna 7% ambao bado hawajaandikishwa. Ndugu Mourice amesema waheshimiwa madiwani ni wenyeviti wa kamati za maendeleo katika kata. Ameomba wadiwani kuhakikisha wanafunzi ambao hawajaripoti shuleni na wanapaswa kuandikishwa mashuleni wanawafuatilia ili wanafunzi hao waandikishwe.
Ndugu Mourice amesema ili kuongeza kiwango cha ufaulu kitaaluma kwa wanafunzi, ni vyema wazazi kuwachangia chakula wanafunzi. Kuna kamati za chakula za wazazi ambazo ndizo zinaweka utaratibu wa kuchangia chakula. swala la uchangiaji wa chakula haliwahusu walimu, ameomba waheshimiwa madiwani kufanya ufuatiliaji wa michango hiyo ili wanafunzi waweze kupata chakula wanapokuwa shuleni.
wanafunzi wa shule ya Msingi wilayani Karatu, katika moja ya Maadhimisho yao wakiomba Wazazi na Walezi kujali haki zao.
Diwani wa kata ya Daa Mhe. Benedicto Modaha amesema bado kuna changamoto za wazazi kupuuza kuchangia chakula shuleni, ili watoto wapate chakula mchana. Amesema upo umuhimu wa watendaji wa serikali kushirikiana na viongozi wa serikali katika kata, ili wazazi wahamasishwe kuchangia vyakula shuleni. Amesema awali walimu wakuu katika kata ya Daa walikuwa wanapingana na watendaji wa kijiji jambo ambalo liliyumbisha ufanisi wa kukusanya michango hiyo. Mhe. Modaha amesema wapo wazazi walikuwa wanakataa kuchangia na hivyo kusababisha watendaji wa vijiji kuingia kwenye gharama za kuendesha kesi. Amesema bado upo umuhimu wa kuendelea kuwapa elimu zaidi na kuhimiza wazazi kuchangia chakula kwa ajili ya watoto, ili watoto waweze kuzingatia masomo vizuri.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa