Kiongozi wafanyabiashara ndugu Charles Goranga amemshukuru mkuu wa wilaya kwa kuendesha kikao na wafanyabiashara. Kikao hicho cha wafanyabiashara kimehusisha watendaji mbalimbali wa Halmashauri na Kuongozwa na mkuu wa wilaya ya Karatu Mhe. Theresia Mahongo. Katika kikao hicho maswala mbalimbali ya wafanyabiashara yalijadiliwa na kupatiwa ufumbuzi na mengine kuchukuliwa kwenda kufanyiwa kazi.
Ndugu. Charles amesema wilaya ya Karatu ni moja ya wilaya pekee yenye baraza la biashara. Amesema kero nyingi za biashara za kikao cha awali zimeshatambuliwa. Baraza la biashara la wilaya litashughulikia kwa kutumia vikundi kazi vya sekta ili kutatua yale mambo yaliyo katika ngazi ya wilaya. Amesema mambo yote yaliyozungumziwa katika kikao cha leo cha wafanyabiashara yatapelekwa kwenye vikundi kazi na baadae yataletwa ili kutoa mrejesho ya namna ya kero hizo zilivyoshughulikiwa.
Amesema baraza la biashara likifanya kazi kwa pamoja na sekta binafsi na sekta ya umma kero zote zitatatuliwa. Ndugu Charles ameomba elimu kuendelea kutolewa kwa wafanyabiashara, amesema sekta binafsi imekuwa haidhaminiwi sana. Sekta za umma ni vyombo vienye maamuzi vikifanya maamuzi yake peke yake hata kama sekta binafsi ikipiga kelele hakuna atakayesikia. Ndugu Charles amesema muundo wa baraza umetoa nafasi sawa za wajumbe kutoka sekta binafsi na sekta ya umma. Hivyo kutoa usawa wa utendaji wa kazi, ameomba kuendelea kushirikiana, amesema kama Halmashauri ikitaka kuweka tozo itoe taarifa kwenye baraza la biashara. Ndugu Charles amesema hiyo itasaidia kuondoa migongano lakini itasaidia kutoa elimu kwa wafanyabiashara.
Ndugu Charles amesema baraza la biashara wa wilaya tayari imeshajadili changamoto ambazo zimefanyiwa mapendekezo tayari kwa kuzipelekea kwenye baraza la biashara la mkoa. Amesema kwenye kujadili changamoto lazima utoe mapendekezo ya chanagamoto hizo ili kufikia muafaka wa pamoja. Kikao cha baraza la mkoa kinatarajiwa kufanyika kati ya tarehe 24/25 mwezi huu.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa