NA TEGEMEO KASTUS
Usimamizi duni wa miradi ndio unaosababisha miradi kujengwa chini ya kiwango na kuchukua muda mrefu kukamilika. Lazima tujenge tabia ya kufanya ufuatiliaji wa mara kwa mara wakati wa ujenzi wa miradi ya maendeleo.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Abbas Kayanda alipofanya ziara ya ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi Lositete na shule ya msingi shikizi Korido na Kituma. Mh. Kayanda umeonesha kutoridhishwa na usimamiaji wa ujenzi wa chumba cha darasa katika shule ya msingi shikizi Korido. Darasa hilo linajengwa kwa fedha za serikali kwa kupitia mfuko wa EPR4.
Katika ziara hiyo Mh. Kayanda ametembelea ujenzi wa jengo la choo katika shule ya msingi Lositete, ujenzi ambao Halmashauri imetoa kiasi cha shilingi million 7.7 kwa ujenzi wa vyoo matundu 5 kwa wasichana na matundu manne kwa ajili ya wavulana. Mh. Kayanda ameoneshwa kutoridhishwa na ujenzi wa vyoo hivyo na ameagiza taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa kufanya uchunguzi wa majengo hayo ya vyoo.
Mh. Kayanda ametoa maelekezo kwa uongozi wa kijiji kukusanya fedha ambazo awali mkutano mkuu wa Halmashauri ya kijiji ulikubaliana kuchangia kwa ajili ya ujenzi wa vyoo hivyo ambavyo havijakamilika katika shule ya msingi Lositete. Sambamba na maelekezo hayo Mlezi wa elimu kata, Injinia wa Halmashauri na Mwalimu Mkuu anayesimamia shule ya Lositete na shule shikizi ya Korido wanapaswa kujieleza kwa maandishi kwa nini wasichukuliwe hatua za kinidhamu kutokana na jinsi walivyosimamia miradi hiyo ya ujenzi wa darasa na vyoo.
Mh. Abbas Kayanda (kushoto) akizungumza kamati ya ujenzi shule ya msingi Lositete
Sambamba na mradi huo Mh. Kayanda ametembelea shule ya msingi Kituma ambayo ni shule shikizi ya Lositete, ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa pamoja na ofisi ambavyo navyo vinajengwa na serikali kupitia mfuko wa EP4R. Amemuelekeza mkandarasi kujenga gebo ya katikati (ukuta unaotenga chumba kimoja na kingine) na kuongeza kasi ya ujenzi wa madarasa ili itakapofika February 10 ujenzi uwe umekamilika ikiwa ni pamoja na uwekaji wa milango na madirisha. Amesema fedha za EP4R zilizotolewa ni pamoja na uwekaji wa madawati, amesema pindi ujenzi wa majengo ya madarasa utakapokamlika madawati na viti viwe tayari vimeshawekwa.
Mh. Abbas Kayanda (kulia) akizungumza na kamati ya ujenzi shule shikizi ya Kituma.
Katika hatua nyingine Mh. Kayanda ameelekeza tathimini ifanyike ili nguvu kazi iliyofanywa na wananchi iweze kufahamika. Amesema ni vyema kuainisha kiasi cha fedha kilichochangiwa na wananchi kwa miradi yote ya ujenzi wa madarasa na choo. Fedha zitakazobaki baaada ya kukamilisha ujenzi madarasa ziweke katika taarifa, Mh. Kayanda anatajia kufanya ziara nyingine ndani ya kipindi cha wiki mbili.
Naye Mkandarasi wa ujenzi wa madarasa fundi Paskali Sixmundi anayejenga darasa katika shule shikizi ya Korido, amesema hakujua kama kunakujenga darasa kwa kutumia ramani, na kufuata (BOQ) licha ya kuwa nayo. Amesema alipopewa tenda ya ujenzi wa darasa katika shule ya msingi shikizi ya Korido aliambiwa ajenge darasa kwa kulinganisha muundo wa darasa lilojengwa awali katika shule hiyo. Amesema kulikuwa na changamoto ya kuleta vifaa vya ujenzi kwenye eneo la mradi kwa kusuasua, jambo ambalo lilifanya ujenzi wa chumba cha darasa kwenda taratibu.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa