NA TEGEMEO KASTUS
Kamati ya ulinzi na usalama ya ikiongozwa na mkuu wa wilaya ya Karatu imetembelea miradi ya EP4R inayojengwa katika tarafa ya Eyasi. Miradi hiyo iko katika hatua tofauti tofauti za ujenzi na inapaswa kukamilika ndani ya kipindi cha miezi mitatu.
Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Abbas Kayanda amewataka wakandarasi kuzingatia muda uliotolewa wa ujenzi wa miundo mbinu ya elimu katika shule hizo. Katika ziara hiyo Mh. Kayanda ametembelea shule ya Msingi Endamaghan ambayo kuna ujenzi wa madarasa mawili na ujenzi wa matundu 20 kumi ya wavulana na 10 ya wasichana vinavyojengwa kwa nguvu za wananchi pamoja na serikali. Katika ziara hiyo Mh. Kayanda alitembelea shule ya msingi Qangdend ambayo ina mradi wa ujenzi wa madarasa mawili.
Mh. Abbas Kayanda akikagua ujenzi wa Msingi wa bweni katika sekondari ya Domel
Mh. Kayanda ametembelea na kujione ujenzi wa bweni la wasichana Mang'ola sekondari linalojengwa kwa fedha za EP4R pamoja na bweni katika sekondari ya Domel. Sambamba na kutembelea ujenzi wa mabweni amekagua ujenzi wa madarasa mawili katika shule ya sekondari Domel yanayojengwa kwa fedha za EP4R na ujenzi wa matundu sita ya choo. Mh. Kayanda amehimiza watendaji kuhakikisha ujenzi wa majengo hayo unaendana na thamani ya fedha zilizotolewa.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa