NA TEGEMEO KASTUS
Familia zenye maisha duni zimeongeza kipato baada ya shirika lisilo la serikali la Food for his children kujenga uwezo kwa wananchi kupitia miradi ya ufugaji na kilimo. Ahueni hiyo ya maisha imesaidia familia duni kujiongezea kipato kwa kupata fedha kwa mahitaji ya wanafunzi na uwezo wa kujenga na kuwekeza katika shughuli mbalimbali za uzalishaji.
Elimu waliopata wananchi ya ujasiramali na kujengewa uwezo wa kufuga mifugo kwa njia za kisasa isambae kwa wananchi wengine. Hayo yamesemwa na Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Abbas Kayanda alipotembelea miradi mbalimbali inayoendeshwa na shirika la food for his chidren katika kijiji cha G-lambo. Amesema Food for his children wanafanya kazi nzuri na wanasaidia serikali katika kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi. Ufagaji wa kisasa unaondoa adhaa ya mfugaji kupoteza muda mwingi wa kuswaga mifugo kutafuta malisho, badalayake anaweza kufuga kwa kwa kuhifadhi kwenye banda na kutumia majani na mabaki ya majani ya mazao kulisha mifugo.
Mh. Abbas Kayanda akikagua miti ya matunda katika shamba la mkulima katika kijiji cha G-lambo
Amehimiza kuweka mkazo katika kilimo cha kisasa amesema wataalamu wa kilimo wanapaswa kuwasaidia wakulima katika kutambua mbegu bora za mazao. Amesema mikakati hiyo itawezekana kama wataalamu watatoa elimu na kufanya ufuatiliaji wa mara kwa mara kwa wakulima. Katika ziara hiyo Mh. Kayanda aliweza kujionea uwezeshaji na uhamasishaji uliofanywa na shirika la food for his children kwa wananchi katika kujihusisha na kilimo cha bustani za mboga katika makazi yao.
Akizungumza kuhusu namna miradi inavyotekelezwa Mkurugenzi wa shirika hilo Bi, Honorina Honorat amesema wanaweka mkazo katika miradi kwa kuhimiza wakulima kuwa na banda la zuri la mifugo. Amesema shirika lilileta mbuzi wa kisasa aina ya sane ambao waliweka utaratibu mzuri wa miradi hiyo kupokelewa na wananchi na kuingia katika umiliki wao. Jambo ambalo limeongeza ari kwa wananchi kujihusisha na ufugaji wa kisasa.
Amesema wananchi wananufaika na ufugaji kwa sababu walikubali kutumia mbinu bora za ufugaji kufuata kanuni za kilimo ikiwa ni pamoja na kuchagua mbegu bora za kupanda na kujihusisha katika upandaji wa miti ya matunda. Sambamba na shughuli hizo shirika limewezesha wananchi kupata elimu ya awali ya usimamizi wa fedha. Bi, Honorati amesema shirika linaweka msisitizo kwa wananchi kujenga vyoo bora ikiwa ni mkakati wa kuboresha mazingira ya kuishi, na kutengeneza vichanja kila nyumba kwa ajili ya kuhifadhi vyombo.
Mh. Kayanda akiwa katika banda la mbuzi la Bi, Fausta Anton
Wakizungumza kuhusu namna walivyonufaika na miradi Bi. Elizabeth Katarina amesema mradi wa kufuga mbuzi umemuwezesha kupata maziwa lita moja au zaidi kwa kila mbuzi wa maziwa na kiwango hicho hutegemea na namna anavyowalisha. Amesema pamoja na kupata maziwa ameweza kumalizia ujenzi wa nyumba ambao awali alikuwa ameshindwa. Hali ya maisha imebadilika ameweza kuongeza idadi ya mbuzi na kujenga banda zuri la mbuzi na la kisasa.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa