Mkuu wa wilaya ya karatu Mhe. Theresia Mahongo amefanya mkutano wa hadhara na wananchi wa kijiji cha Matala. Mkutano huo ulilenga kubaini watu wanaojihusisha na uhalifu katika maeneo ya Matala, Yaeda ya chini na kuhatarisha amani na usalama kwa wananchi.
Mhe. Theresia Mahongo amesema hatakubali mambo ya uhalifu yatokee kwenye eneo lake, amesema wahalifu wengi wapo katika kijiji cha Matala. Mhe. Mahongo amewapongeza wananchi wanaoendelea kutoa ushirikiano kwa serikali dhidi ya uhalifu unaofanyika, amesema Mhalifu mmoja alikamatwa katika kijiji cha Yaeda ya chini lakini pia msako umeendelea kimya kimya na katika msako huo ng’ombe mmoja ambaye alikuwa ameibwa alikamatwa mnada wa Meatu.
Mhe.Mahongo amesema ameambiwa kwamba wahalifu wamekuwa wakisaidiwa na baadhi ya wananchi na watendaji wa serikali. Ameomba wananchi kuwakataa watu wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu kama ukoma. Mhe. Mahongo amewaongoza wananchi kupiga kura za siri ili kubaini na kujiridhisha kwa kupata majina ya watu wanaojihusisha na shughuli za uhalifu. Mhe. Mahongo amewaambia hata alipofika kwenye kijiji amekuta kuna mwananchi amejeruhiwa na mwanachi mwenzake vibaya sana. Amesema lazima hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi yake, amesema Mtuhumiwa amekuwa na matatizo ya kuogofya katika kijiji cha Matala. Amesema anataka kumuona askari atakayemuachia huyo Mhalifu tena ili aendelee na shughuli za kuhatarisha amani na usalama katika kijiji cha Matala.
Mwananchi akipewa msaada wa kupiga kura ya siri kubaini watu wanaojihusisha na Uhalifu Matala.
Mhe. Mahongo amesema ameambiwa kuna watu wanavamia vibanda usiku na kubomoa ikiaminika wanakula wali, ndizi, wanakula maandazi. Amesema mtu anayefungua mlango wa mwenzake bila ufunguo ni mwizi, ameonya watu wanaofanya hivyo muarubaini wao unakuja. Amesema kuna Sungusungu katika kijiji cha Matala lakini Sungusungu ya Matala haifanyi vizuri. Amesema Sungusungu ni watu wanaofanya ulinzi shirikishi, amesema lazima Sungusungu wafuate sheria amehimiza wananchi kukaa na kupanga viwango vya faini. Amesema kwa namana wanavyotoza fani kwa sasa laki tatu si sawa, Mhe Mahongo amesema Mkuu wa polisi atakwenda kuwapa mafunzo Maalumu Sungusungu hao kijijini Matala ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi.
Mhe. Mahongo amewaelekekeza viongozi wa kijiji kujiandaa ili waweze kufanya zoezi la mgambo kwa vijana. Amesema kuna Mgambo anaitwa Lukasi amesema ameshamvua cheo cha Mgambo na wamemchukulia cheti chake, amesema kama Lukasi anakuja Matala akae kama Mwanachi wa kawaida na sio kama Mgambo. Amesema tuhuma Mbalimbali ndio zilizomvua cheo hicho huko Mang’ola ikiwa ni pamoja na rushwa.Amesema Kuna kijana anaitwa Jafari naye anashirikiana na Mkuu wa kituo cha Ibaga wilaya ya Mkalama kukamata wananchi bila utaratibu. Mhe. Mahongo amemuonya Mwanamgambo Jafari kuacha tabia hiyo mara moja.
Mhe. Mahongo amesema swala la usalama ni kitu cha kwanza kuliko mambo mengine yote, ameomba wananchi kujitolea na kuanza kujenga kituo cha polisi kijiji cha Matala. Mhe. Mahongo ametoa Mifuko Ishirini kwa kuanzia, ili kuanza kujenga kituo cha polisi. Ameomba wananchi wamuunge mkono katika ujenzi wa kituo cha polisi Matala. Amesema kujenga kituo cha polisi kutawezesha askari kuwa na silaha, amesema kujenga kituo cha polisi ni muhimu kwa sababu askari watapata sehemu ya kuhifadhi silaha. Amesema kwa hali ilivyo kijiji cha Matala kinahitaji kuwa na kituo chenye Maaskari angalau wanne kwa kuanzia . Ameomba wananchi kuanza kutoa mchango wa shilingi elfu kumi, amemuelekeza Mtendaji wa kijiji kuandaa kibali cha kukusanya mchango na kukukipeleka ofisi ya Mkuu wa wilaya na ameahidi kukipitisha kibali hicho, kwa sababu kila mwananchi kwenye mkutano wa hadhara amekubali kuanza ujenzi wa kituo cha Polisi.
Mwananchi akiwa anasaidiwa vyombo vya ulinzi katika zoezi la upigaji wa kura za siri
Awali ndugu Abbasi Kayanda amesema kwenye Mkutano na wananchi wa kijiji cha Matala kwamba kumekuwa na matatizo ya wizi wa mifugo. Amesema jambo hilo linakera, katika vijiji 57 vya wilaya ya Karatu kijiji cha Matala kimekuwa kikiripotiwa matukio ya wizi mara kwa mara. Ndugu Kayanda amesema katika msako uliofanywa katika mnada katika Wilaya ya Meatu, ng’ombe walioibwa katika kijiji cha Yaeda chini wilaya ya Mbulu walipatikana mnada wa Meatu.
Ndugu Kayanda amesema pamoja na kufanya mkutano tunataka kufahamu tatizo liko wapi ?? Amesema hata kama kuna tatizo la wizi, mwizi hawezi kutoka mbali kama hakuna mwizi anayeshirikiana naye eneo la karibu. Amesema wananchi wamekuwa wakiona haya na kuwataja watu wanaojihusisha na shughuli za uhalifu katika kijiji cha Matala. Ndugu kayanda amesema mkutano huo unalenga kupata ufumbuzi wa matatizo ya uhalifu yanayofanyika katika kijiji cha Matala
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa