Kamati ya fedha imetembelea jengo la utawala la shule ya sekondari Endabash na jengo la utawala la shule ya sekondari Kansay. Kamati imeridhishwa na kasi ya ujenzi wa majengo hayo yaliyo katika hatua za mwisho kukamilika.
Mhe. Mwenyekiti Jublate Mnyenye amesema kazi ya ujenzi inaenda vizuri; ameelekeza kamati ya ujenzi ya shule ya sekondari Endabash, kuendelea kuhusisha wananchi ili kujitolea nguvu kazi. Amesema kuna baadhi ya kazi wananchi hawana budi kuhusishwa ili fedha ziweze kutosheleza katika ujenzi kama kuleta baadhi ya vifaa mathalani mchanga, maji na kokoto. Kwa mujibu wa Mwalimu James Godson amesema jengo hilo la utawala la shule ya Endabashi limepewa fedha kiasi cha Million 50 za EP4R na mpaka sasa kiasi cha fedha zilizotumika ni shilingi Million 24 na elfu 67 na mia nne na salio lilobakia ni million 25 laki 9 na 32 na mia sita. Mwl Godson amesema wananchi walifanya jitihada za awali kwa kujitolea nguvu kazi katika kuchimba msingi na kuweka mawe.
Katika ujenzi wa jengo la utawala la Shule ya sekondari Kansay, kamati ya fedha imetoa muda wa ndani ya wiki mbili jengo hilo liwe limekamilika. Mwl Mkuu Shauri Amnaay amesema wamepewa kiasi cha shilingi million 10 kutoka Halmashauri tarehe 15 mwezi January. Jengo limewekwa rafu ya chini na kupigwa plasta ndani na nje. Jengo litawekewa vioo kwenye madirisha na kuweka milango. Kamati hiyo haikukuta mafundi wakiendelea na kazi lakini Mwl Shauri amesema fundi aliyepewa mkataba aliugua jambo ambalo llimesababisha kuchukua mda mrefu, umaliziaji wa jengo la utawala la shule ya Kansay.
Kamati ya fedha ilitembelea jengo la maabara la shule ya sekondari Kansay, ambalo nalo pia limepewa million 10 lakini ujenzi haujakamilika. Fedha hizo zilitolewa mwaka wa fedha mwaka 2017/2018, Mhe. Jublate ametoa maelekezo kwa Afisa elimu kuchukua hatua za kisheria kwa kamati ya ujenzi ya kijiji. Amesema haiwezekani kiasi hicho cha fedha kishindwe kumaliza jengo la chumba kimoja cha maabara.
Muonekano wa jengo la utawala kwa nje shule ya sekondari Endabash.
Muonekano wa jengo la utawala kwa nje shule ya sekondari Kansay.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa