Shule ya sekondari Dr. Wilbroad Slaa na Shule ya sekondari Endala zimetembelewa na kamati ya fedha ya Halmashauri. Kamati hiyo ilienda kutembelea kuona namna shule hizo zilivyotumia fedha za ujenzi wa vyoo zilizopelekwa katika shule hizo pamoja na ukarabati wa bweni.
Kamati ilijionea ujenzi wa vyoo vya matundu kumi vya wasichana katika shule ya sekondari Dr .Wilbroad Slaa. Lakini pia ikajionea changamoto ya mahitaji mapya ya ujenzi wa vyoo vingine vya wavulana katika shule ya Dr. wilbroad Slaa. Mhe. Jublate Mnyenye amesema million sita iliyotolewa na Halmashauri imetumika vizuri. Ameelekeza mwenyekiti wa kijiji na mkuu wa shule kuhusisha wananchi ili vyoo hivyo viweze kumalizika na vianze kutumika haraka. Lakini pia amesema milion 15 za ukarabati wa bweni na vyoo katika shule ya sekondari Endala zimetumika vizuri.
Mhe Lucian amesema wamejenga maliwato katika shule ya sekondari Dr.Wilbroad Slaa nje shimo ili kuepusha adhaa ya maliwato kudidimia pindi mvua inaponyesha. Vyoo hivyo vimejengwa kwa ubora, shimo limekwenda chini futi 16 na uwezekano upo shimo likijaa kuondoa taka. Lakini shimo hilo limejengwa kwa nguzo tatu za nondo lakini pia shimo limewekewa mgawanyo wa vyumba ili kulipa uimara.
Ziara hiyo ya kamati ya fedha ililenga kufanya tahimini na kujiridhisha namna fedha za Halmashauri zilivyotumika. Kamati ya fedha imeridhika na matumizi ya kiasi hicho cha fedha kilivyotumika kwa shule zote mbili.
Mwenyekiti ndugu Michael Harshim wa Basodawich amesema wamechangisha kila mwanachi kiasi cha shilingi 5000, na ujenzi wa shimo hilo la pembeni umegharimu million 14. Hizo ni fedha tofauti na ujenzi wa matundu ya choo zilizotolewa na halmashauri. Wanampango pia wa kujenga matundu ya vyoo vya wavulana kwa kutumia shimo hilo walilolitengeneza.
Naye Mwl Mkuu Joshua Sabbas amesema shule ya sekondari Endala imepewa shilingi million 15, kwa ajili ya kuweka ripu ndani kwenye bweni la wasichana na kuweka sakafu chini. Walitumia fedha hizo pia kujenga matundu ya vyoo vinne na mabafu sita pamoja na sehemu ya uzio. Shule hiyo ilijengwa kwa ufadhili wa Marafiki wa Mhe. Lucian kutoka Belgium kwa gharama ya zaidi ya million 860 na baadae kukabidhiwa Halmashauri.
Kamati ya fedha ikikagua bweni la wasichana shule ya sekondari Endala.
kamati ya fedha ikagua choo shule ya sekondari Dr, Wilbroad Slaa.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa