NA TEGEMEO KASTUS
Taasisi ya kuzuia na kupambana na rusha TAKUKURU wilayani Karatu, kufanya uchunguzi wa jengo la choo Mnada wa Qangdend. Uchunguzi huo unalenga kujiridhisha kama thamani ya miundo mbinu inaendana na kiasi fedha kilichotolewa katika ujenzi wa maliwato hayo.
Maelekezo hayo yametolewa na Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Abbas Kayanda baada ya kufanya ziara katika eneo hilo la maliwato. Ameelekeza uongozi wa kijiji kabla ya taraehe 5 mwezi wa tisa, kuhakikisha ukarabati wa milango na madirisha ambayo haipo iwe imewekwa na jengo hilo lianze kulindwa ili miundo mbinu hiyo iwe katika hali ya usalama. Ujenzi wa Maliwato hayo una kadiriwa kugharimu Halmashauri kiasi cha shilingi Million 8. Baada ya ujenzi jengo hilo lilikabidhiwa uongozi wa Halmashauri ya kijiji cha Qangdend ili waweze kulisimamia na kuliendeleza.
Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Abbas Kayanda (kulia) akikagua ujenzi wa madarasa unaoendelea shule ya sekondari Domel.
Mh. Kayanda ametembelea ujenzi wa madarasa mawili ya shule ya sekondari Domel pamoja na Ofis ya Walimu ambayo ameelekeza mpaka kufikia tarehe 20 mwezi huu ujenzi wake uwe umemalizika. Madarasa hayo yanajengwa kwa nguvu za wazazi.
Mh. Abbas Kayanda akikagua kifuniko cha juu cha tanki la kuhifadhia maji.
Mh. Kayanda ametembelea ujenzi wa bweni linalojengwa na Tasaf katika shule ya sekondari ya Qangdend na kujionea maendeleao ya ujenzi. Mh. Kayanda ameelekeza Mratibu wa Tasaf wilaya kuhakikisha mradi unakamilika kwa mujibu wa Mkataba.
Mh. Kayanda ametembelea pia ujenzi wa eneo la kunyweshea mifugo, mradi bado uko kwenye hatua za ukamilishaji wa ujenzi, umejengwa katika eneo la Qangdend. Mradi huo ukikamilika utasaidia wananchi wa Qangdend kupata sehemu ya kunyweshea mifugo. Mh kayanda amesisitiza kwamba miradi yote inayojengwa ni lazima iendane na thamani ya fedha iliyotolewa.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa