NA TEGEMEO KASTUS
Huduma ya maabara, jengo la mama na mtoto na chumba cha kujifungulia ni vipaombele muhimu katika kutoa huduma za afya kwa wananchi. Ujenzi wa zahanati ya Kijiji cha Huduma unaendelea baada ya serikali kutoa fedha shilingi milioni hamsini kwa ajili ya ujenzi. Ujenzi wa zahanati hiyo ukikamilika utawaondolea adha wananchi ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya Rhotia.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Abbas Kayanda alipotembelea zahanati ya huduma kujionea maendeleo ya ujenzi wa zahanati hiyo. Amesema lazima kamati ya ujenzi ihakikishe huduma ya maji na umeme inakuwepo katika zahanati. Amesema lazima kamati ya ujenzi isimamie fedha za ujenzi vizuri ili ubora wa majengo uendane na thamani ya fedha iliyotolewa.
Mh. Abbas Kayanda akiwa katika zahanati ya kijiji cha huduma
Katika hatua nyingine Mh. Kayanda ametembelea zahanati ya kijiji cha Kilimatembo ambacho kimetengewa kiasi cha million kumi na Halamashauri ya wilaya ya Karatu fedha ambazo ziko kwenye bajeti ya mwaka huu wa fedha. kiasi hicho cha fedha kitatumika kumalizia ujenzi wa jengo la zahanati ya kijiji cha Kilimatembo. Ikiwa ni pamoja na kuweka milango na ceiling board, hatua hizo zikienda sambamba na ujenzi wa choo na kichomea taka.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti Mwenyekiti wa kijiji cha huduma Ndg. Leornad Paulo amesema watazingatia maelekezo yaliyotolewa na serikali, amesema kabla ya ziara hiyo changamoto iliyokuwa inawasumbua ni ubebaji wa mchanga ambayo nayo imeshapatiwa ufumbuzi. Amesema kazi itaenda kwa kasi kwa sababu tayari wataalamu wameshaelekeza eneo la kujenga kichomea taka na eneo la kujenga maliwato ya nje.
Naye Mwenyekiti wa kijiji cha Kilimatembo ndg. Nicodemus Said amesema watafanya kila linalowezekana kuhakikisha ujenzi huo unakamilika na wananchi wanaanze kupata huduma za afya katika zahanati ya Kilimatembo. Amesema watatumia msitu wa kijiji ili kupata mbao ambazo zitatumika kuweka milango kwenye zahanati.
Mh. Abbas Kayanda akiwa katika zahanati ya kijiji cha kilimatembo.
matukio katika picha wakati ziara katika zahanati ya kilimatembo.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa