Kamati ya fedha ya Halmashauri imetembelea zahanati ya kijiji cha Genda, kujione marekebisho ya majengo ya zahanati. Majengo hayo yamejengwa miaka mingi iliyopita, yamepata fedha za Halmashauri kwa awamu mbili ili kufanyiwa ukarabati.
Mhe. Jublate Mnyenye amesema ukarabati wa majengo utekelezaji wake umefanyika vizuri lakini pia kwa upande mwingine haujafanya kazi vizuri. Majengo ya zahanati hiyo yamepewa million 10 awamu ya kwanza na wamepewa milioni 10 kwa awamu nyingine. Lengo la kufanya ukarabati huo ni kuwekea miundo mbinu mizuri ili iendele kuhudumia vijiji vingine vya jirani. Pamoja na urekebishaji huo bado kuna udhaifu wa fundi anayekarabati jengo hilo kwa kushindwa kuweka mashimo kwenye msingi ili udongo uweze kupumua. Mhe. Mnyenye amesema sakafu inaweka mpasuko kutokana na kukosa mashimo ya kupumua.
Mwenyekiti wa ujenzi zahanati ya kijiji cha Genda Ndugu Paskali amesema kamati ya ujenzi imekuwa haishirikishwi. Hivyo ujenzi huo kuendelea bila ya kamati ya ujenzi; licha ya vifaa kuagizwa na kuletwa eneo la ukarabati wa mradi bila wajumbe kujua hatua za manunuzi, lakini pia namna ujenzi huo unavyofanyika. Wajumbe hao wamemtuhumu Mganga wa kituo hicho Adiael Wilson kwa kufanya shughuli za ukarabati bila kuhusisha kamati ya ujenzi. Kamati hiyo ya fedha imetilia shaka kasi ya ujenzi wa kituo hicho na kumuomba Mganga Mkuu wa wilaya kufuatilia swala hilo kwa undani. kamati hiyo imeelekeza Wajumbe wa kamati ya Ujenzi wa majengo hayo yanayokarabatiwa na Halmashauri kuhakikisha malipo ya mwisho ya mafundi yanalipwa baada ya ukarabati kukamilika na majengo kuwa katika hali nzuri. lakini pia wameagiza kupewa nyaraka, na vielelezo vyote vya namna ukarabati huo unavyoendelea.
Wajumbe wa kamati ya fedha, wakikagua moja ya jengo linaloendelea kukarabatiwa na mafundi.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa