Na Tegemeo Kastus
Madawati, Meza na viti vilivyokuwa vimepelekwa kukarabatiwa na matokeo yake kutelekezwa kwa fundi Seremala kwa muda wa miaka miwili bila kufanyiwa matengenezo vyarudishwa shule ya sekondari Gyekrum Lambo.
Maelekezo hayo yametolewa na Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Abbas Kayanda baada ya kufanya ziara ya kushitukiza katika kijiji cha G-Lambo kijiweni na kukuta madawati 26 meza 17 na viti 16 vilivyokuwa vimewekwa katika stoo ya fundi Wilbrod Qabi Hayshi. Viti hivyo vimekaa muda mrefu kutokana na shule ya sekondari G-Lambo kushindwa kukamilisha madai ya fedha kiasi cha 12,8000 zilizokuwa zinadaiwa na fundi seremala. Wilbrod Qabi Hayshi aliyekuwa akikarabati thamani hizo.
Mh. Kayanda amemuelekeza Mkuu wa shule ya sekondari G-lambo kuhakikisha viti meza pamoja na madawati hayo yanarejeshwa shuleni. Amesema madawati hayo yatengenezwe yakiwa shuleni ndani ya kipindi cha siku kumi na nne na shule ilipe deni fundi seremala Wilbrod Qabi Hayshi ndani ya kipindi cha siku kumi na nne.
Katika hatua nyingine Mh. Kayanda ametembelea ujenzi wa vyumba vya madarasa mawili pamoja na ofisi ya walimu katika shule ya Baray Khusumay ujenzi unaojengwa kwa nguvu za wananchi wakishirikiana na serikali ya kijiji. Mh. Kayanda ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa madarasa na ameelekeza Halmashauri kuhakikisha inakamailisha upauzi wa majengo hayo ndani ya mwezi huu.
Mh.Abbas Kayanda (aliye mbele) akikagua ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya sekondari Dkt. Wilbroad na Baray Khusumay
Mh. Kayanda ametembelea pia ujenzi wa vyumba vya madarasa unaojengwa kwa nguvu za wananchi pamoja na serikali ya kijiji katika shule ya sekondari Dkt. Wilbroad Slaa. Sambamba na kukagua ujenzi huo Mh. Kayanda ametembelea na kukagua ujenzi wa bweni la wasichana linalojengwa na wafadhili katika shule hiyo. Ameelekeza mafundi kuongeza kasi ya ujenzi ili bweni hilo liweze kukamilika kwa wakati.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa