Walimu wakuu na Afisa elimu wametakiwa kujieleza kimaandishi na kuwasilisha maelezo Ofisi ya Rais Tamisemi juu ya kutofautiana kwa gharama za ujenzi wa mabweni katika shule za sekondari Mang’ola na Domel hasa ikizingatiwa fedha na ramani ya michoro kama hiyo imekamilisha ujenzi katika meneo mengine.
Maelekezo hayo yametolewa Naibu waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Mh. David Silinde alipofanya ziara ya siku moja na kugundua kushindwa kukamilika kwa mabweni shule za sekondari katika tarafa ya Eyasi Karatu. Mh. Silinde ametoa muda wa siku tatu kwa watumishi hao kujieleza kwanini ujenzi haujakamilika na ametoa maelekezo kwa Injinia wa wilaya kueleza kwanini BOQ imekuwa na gharama kubwa sana tofauti na fedha zilizotolewa na serikali. Samba na maelekezo hayo Mh. Silinde ametaka uchunguzi ufanyike ili kujiridhisha uhalisia wa gharama zilizotumika katika ujenzi uliofanyika.
Mh. Silinde amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Magufuli anatoa fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya elimu lakini tatizo limekuwa usimamizi dhaifu ngazi ya chini juu ya namna wanavyosimamia ujenzi. Amewataka watendaji kukamilisha ujenzi ili watoto waweze kuingia na ameahidi kurudi kutembelea mwezi wanne.
Mh. David Silinde akikagua ujenzi wa moja ya bweni katika tarafa ya Eyasi Karatu
Akizungumza wakati wa ziara hiyo Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Abbas Kayanda amemshukuru Naibu waziri ofisi ya rais Tamisemi kwa ziara aliyoifanya wilayani Karatu. Mh. Kayanda ameagiza taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa kuanza kuchunguza gharama za ujenzi wa shule hizo ili kubaini kama kuna matumizi mabaya ya fedha katika ujenzi wa miundo ya elimu katika shule hizo.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa