Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo ametembelea mradi wa maji katika kijiji cha Umbagw pamoja na kuzungumza na wananchi. Mradi huo wa maji umetengenezwa na shirika la world vision Tanzania.
Mhe. Gambo ametembelea eneo la mtambo wa maji unaoendeshwa kwa nguvu za jua pamoja na kupewa maelekezo ya kitaalam namna mradi unavvyofanya kazi. Zoezi hilo lilienda sambamba na kupanda miti iliyozunguka eneo lillojengwa mtambo wa kuzunguka maji Mhe. Gambo amelipongeza shirika la world vision kwa kusaidia kutengeneza miundo ya maji na watu kupata maji katika kijiji Umbagw tarafa ya Endabash. Amesema world vision wanashirikiana vizuri na serikali ndio maana miradi inatekelezeka. Mkuu wa mkoa amesema wataendelea kufuatilia na kuhakikisha pampu ya maji kijiji cha Kambi ya Faru inapatikana kwa sababu fedha tayari ilishatengwa kwa ajili ya kununua pampu mpya. Amesema mradi wa maji Kansay unaogharimu kiasi cha shilling million 139 ili ukamilike, amesema atawasiliana na vyombo husika kuhakikisha mradi huo unakamilika.
Mkuu wa Mkoa mhe. Mrisho Gambo akiapanda mji katika eneo la mradi wa mashine za kusukuma maji.
Danieli Kirima mwakilishi wa world vision amesema furaha yao ni kuona watu wanakunywa maji safi na salama. Amesema world vision ni wadau wa wananchi na serikali, tayari wameandaa andiko la awali ambalo litasadia kupata fedha kiasi cha billion 4 kujenga miundo mbinu ya maji Laja na vijiji vingine vinavyozunguka eneo hilo. Ameomba wananchi kuendelea kuvuta subira, wakati shirika likijiandaa kwa utekelezaji wa mradi huo baada ya ombi la andiko la utekelezaji kupita.
Naye mukazi wa kijiji cha Umbagw Petrolina Nicodem ameshukuru serikali kwa kuwapatia maji katika kijiji cha umbagw. Amesema walikuwa wanatembea umbali zaidi ya km12 kufuata maji, amesema umbali wa km 12 ukizidisha kwa siku 360 za mwaka ni umbali mrefu sana. Ameomba serikali kuongeza (DP) Pampu za za maji ili vitongoji mbalimbali katika vijiji hivyo viweze kupata maji.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa