Mtaa ni eneo ambalo hutokana na kugawanywa kwa maeneo ya kata za mijini, Mamlaka ya Mji ndiyo inayoamua idadi ya kaya ambazo zitaunda Mtaa mmoja. Uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika tarehe 24/Nov/2019 ulichagua wenyeviti wa mitaa. Chama cha mapinduzi kiliibuka mshindi wa jumla kwa kutwaa wenyeviti wote wa mitaa katika maeneo mbalimbali katika Mamlaka ya mji mdogo wa Karatu.
Zoezi la makabidhiano ya ofisi kati ya wenyeviti waliomaliza muda wao na wenyeviti wa sasa linaendelea maeneo mbalimbali. KANUNI TARATIBU ZA SHERIA ZA UENDESHAJI WA KIJIJI NA KITONGOJI NA MTAA zilizotolewa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa mwezi wa kumi mwaka elfu mbili. Zinaelekeza kwamba mtaa huongozwa na mwenyekiti wa mtaa na Mwenyekiti wa mtaa huchaguliwa na wakazi wa mtaa wenye umri wa miaka 18 na kuendelea. Uchaguzi wa mwenyekiti wa mtaa hufanyika kila baada ya miaka mitano kwa mujibu wa taratibu za uchaguzi wa serikali za Mitaa.
Kanuni zinaelekeza Mwenyekiti wa Mtaa na atakuwa ndiye kiongozi Mtendaji Mkuu kwenye Mtaa. Ataongoza vikao vyote vya kamati ya mtaa na kikao cha wakazi wote wa mtaa. Kiongozi wa mtaa anapaswa kutunza rejesta ya wakazi wote wa mtaa ambayo itaonyesha; taaarifa muhimu za kila mkazi, walipa kodi wa mtaa, umri na jinsia ya kila mkazi, vizazi na vifo vinavyotokea kwenye mtaa, hii ni kwa mujibu wa kanuni za taratibu za sheria za uendeshaji wa kijiji na kitongoji na mtaa zilizotolewa na Ofisi ya Rais Tawala za serikali za Mitaa October (2000)
Mwenyekiti wa mtaa atasimamia ulinzi na usalama wa watu na mali zao kwenye mtaa, kwa kuhakikisha kuna idadi kutosha ya Wanamgambo/Sungusungu kwenye mtaa. Wahalifu wanafikishwa kwenye mabaraza ya kata kwa kushirikiana na kamati ya Mtaa, kuweka utaratibu wa ulinzi nyakati za usiku. Mwenyekiti wa mtaa anapaswa kusuluhisha migogoro midogo midogo isiyostahili kushughulikiwa na mabaraza ya kata au mahakama kama vile; Ugomvi wa kawaida kati ya mke na mume, ugomvi ambao hauhusu mambo ya talaka. Madai ya kawaida yanayotokana na kukopeshana fedha na vitu vidogo vidogo kati ya wakazi wa mtaa na kutaoelewana kwa majirani wa mtaa. Hii ni kwa mujibu wa kanuni za taratibu za sheria za uendeshaji wa kijiji na kitongoji na mtaa zilizotolewa na Ofisi ya Rais Tawala za serikali za Mitaa October (2000)
Kanuni zinaelekeza Mwenyekiti anatakiwa kuhakikisha ulipaji wa kodi na ushuru mbalimbali wa Halmashauri, na kusimamia utekelezaji wa kanuni za afya ikiwa ni pamoja na kuhakikisha; kampeni za afya kitaifa zinatekelezwa, mazingira ya mtaa ni msafi, kila mkazi wa mtaa ana choo, karo la maji machafu na shimo la kutupia taka. Taarifa ya mlipuko wa mgonjwa ya kuambukiza kama kipindupindu inatolewa taarifa.
Mwenyekiti wa mtaa atahakikisha kila mtoto mwenye umri wa kwenda shule anaandikishwa na kuhudhuria hadi amalizapo; kwa kushirikiana na kamati za shule kupata taarifa za mahudhurio ya watoto walio kwenye mtaa wake, kuwahimiza wazazi kulipa ada na michango ya shule, kufanya utaratibu kwa kushirikiana na kamati ya mtaa kwa kuhakikisha kuwa watoto ambao hawana wazazi au walezi wanasaidiwa kuhudhuria masomo. Mwenyekiti wa mtaa anapaswa kuhamasisha elimu elimu ya watu wazima; kuhamsisha wakazi wa mtaa kushiriki katika shughuli za kujitegemea na atatekeleza kazi nyingine atakayopewa na Halmashauri.
kanuni za taratibu za sheria za uendeshaji wa kijiji na kitongoji na mtaa zilizotolewa na Ofisi ya Rais Tawala za serikali za Mitaa October (2000) zinataka kila mtaa kuwa na kamati, kamati ya mtaa ina wajumbe wasiozidi sita ambao wawili kati yao lazima wawe wanawake. Wajumbe wa kamati ya mtaa watachaguliwa na wakazi wa mtaa kutoka miongoni mwao katika uchaguzi wa serikali za mitaa ambao hufanywa kwa mujibu wa taratibu za uchaguzi wa viongozi wa serikali za zinazoandaliwa na waziri mwenye dhamana ya serikali za mitaa.
Kanuni za taratibu za sheria za uendeshaji wa kijiji na kitongoji na mtaa zilizotolewa na Ofisi ya Rais Tawala za serikali za Mitaa October (2000) zinaeleza kazi za kamati; ni kutekeleza sera za Halmashauri, kutoa ushauri kwa Halmashauri kuhusu mipangao ya maendeleo ya shughuli za mitaa, kutoa ushauri kwa kamati za maendeleo za kata kuhusu mambo yote yahusuyo amani na ulinzi kwenye mtaa, kuweka kumbukumbu sahihi kuhusu taarifa za wakazi wa mtaa, kufanya jambo jingine lolote kama itakavyoagizwa na kamati ya maendeleo ya kata.
Mkutano wa wakazi wa mtaa utaitishwa na Mwenyekiti wa mtaa mara moja kila mwezi, mwenyekiti wa mtaa ataitisha mkutano wa dharura endapo ataona kuna haja ya kufanya hivyo. Mkutano wa wakazi wa mtaa unaweza kuzungumzia; kuwasilisha maagizo na matumizi ya mkutano wa kamati ya maendeleo ya kata. Jambo lolote ambalo linahitaji ushirikishwaji, jambo lolote ambalo lina maslahi kwa wakazi wa mtaa ambapo wakazi wamtaa wanapaswa kutoa mawazo yao mathalani endapo kunatakiwa kuanzishwa mradi Fulani kwenye eneo la mtaa. Shughuli yeyote ya kimaendeleo inafanyika kwenye mtaa inapaswa kutekelezwa kwa nguvu kazi. Kueleza maagizo yoyote ambayo yanatakiwa kutekelezwa kwenye ngazi ya mtaa. Mwenyekiti anatakiwa kuweka mikakati ya utekelezaji wa maagizo yoyote yanayotolewa na mamlaka za juu. Muhtasari wa kikao chochote kwenye kikao cha mtaa huwasilishwa kwenye kikao cha kamati ya maendeleo ya kata.
kanuni za taratibu za sheria za uendeshaji wa kijiji na kitongoji na mtaa zilizotolewa na Ofisi ya Rais Tawala za serikali za Mitaa October (2000) zinasema mwenyekiti wa mtaa husika ana madaraka kwa muda wa miaka mitano. Wakazi wa mtaa wanaweza kumuondoa mwenyekiti wao madarakani kabla ya kipindi chake cha madaraka kwa sababu kama; wananchi kupeleka malalamiko kwa afisa mtendaji wa kata yaliyosainiwa na na nusu ya wakazi wa mtaa wenye umri wa miaka kumi na nane na kuendelea. Malalamiko yanayotolewa ili yaweze kujadiliwa kwenye kikao cha wakazi wa mtaa ni lazima yawe na tuhuma mahususi zenye ushahidi wa kutosha. Mtendaji wa kata anapoyapokea malalamiko hayo na kuridhika kwamba yamekamilika na yana ushahidi kamili atayapokea rasmi.
kanuni za taratibu za sheria za uendeshaji wa kijiji na kitongoji na mtaa zilizotolewa na Ofisi ya Rais Tawala za serikali za Mitaa October (2000) mara apatapo malalamiko hayo kabla ya kupita siku saba, Afisa mtendaji wa kata, atandaa mkutano wa dharura wa wakazi wote wenye umri wa miaka kumi na nane na kuendelea. Kabla ya mkutano kuanza wakazi waliohudhuria watamchagua mwenyekiti wa kuendesha mkutano huo kutoka miongoni mwao. Afisa mtendaji kata atasoma tuhuma na ushahidi wote uliotolewa dhidi ya mwenyekiti wa mtaa na baada ya maelezo ya mtendaji wa kata, Mwenyekiti anayetuhumiwa atapewa fursa ya kujitetea mbele ya mkutano huo na maelezo na vilelezo kama anavyo. Baada ya kutafakari kwa kina utetezi wa Mwenyekiti anayetuhumiwa, wakazi watapiga kura ya kuamua kumuondoa mwenyekiti madarakani au la. Endapo kura zitakazopigwa dhidi ya mwenyekiti anayetuhumiwa zitakuwa ni theluthi mbili au zaidi ya kura zote zilizopigwa basi mwenyekiti huyo atakuwa ameondolewa madarakani. Kura za kumuondoa mwenyekiti madarakani zitakuwa kura za siri.
Kanuni za taratibu za sheria za uendeshaji wa kijiji na kitongoji na mtaa zilizotolewa na Ofisi ya Rais Tawala za serikali za Mitaa October (2000) Mwenyekiti ambaye ataondolewa madarakani ana haki ya kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa mkutano wa wakazi kwa mkuu wa wilaya ndani ya siku thelathini. Baada ya siku thelathini mwenyekiti wa aliyetuhumiwa atakuwa amepewa ruhusa ya kukata rufaa Afisa mtendaji wa kata ataarifu Halmashauri ya mji kuwepo kwa nafasi hiyo ya wazi ili Halmashauri ifanye utaratibu wa uchaguzi.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa