NA TEGEMEO KASTUS
Wilaya ya karatu ina maeneo 37 ambayo yanapaswa kufikiwa na mradi wa umeme vijijini (REA). Mpaka sasa kuna maeneo zaidi ya 20 katika wilaya ya Karatu ambayo umeme wa REA haujafika, wakala wa umeme vijijini kupitia kampuni ya NIPO wanatarajia kufikisha umeme kila sehemu ambayo haiujafikiwa na umeme wa REA ndani ya kipindi cha miezi mitatu.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Abbas Kayanda wakati akizungumza na wananchi alipotembelea zahanati ya Ngaibara. Amesema anafahamu kuna sehemu ambazo umeme wa Rea haujafika kama kijiji cha Laja, kitongoji cha Baray, Mbuyuni ni miongoni mwa maeneo ambayo umeme wa Rea haujafika . Amesema umeme wa REA utafika maeneo yote wilayani Karatu, Mh. Kayanda ameomba wananchi kutumia mafundi ambao wanatambulika na Tanesco wakati wa kuweka umeme nyumba zao ili kukwepa mafundi vishoka ambao wanaweza kufanya kazi hizo bila ufanisi. Amewaambia wananchi wanatakiwa kujaza fomu za kujaza umeme ili wakati wa kusambaza umeme uweze kuwekwa katika makazi yao. wakati huo huo Mh. Kayanda ametoa maelekezo kwa watendaji wanaosimamia ujenzi wa zahanati ya Ngaibara kuhakikisha miundo mbinu ya maji iwe tayari mpaka kufika alhamisi. Mh.kayanda ametoa siku 10 kuhakikisha ujenzi wa matundu ya choo katika zahanati ya Ngaibara uwe umekamilika.
Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Abbas Kayanda akikagua ujenzi wa maabara ya kituo cha afya Endabash.
Mh. Kayanda ametembelea ujenzi wa jengo la maabara katika kituo cha afya Endabash na amejionea ujenzi wa msingi wa maabara. Ujenzi wa maabara utachukua muda wa miezi mitatu mpaka kukamilika kwake na utarajia kuboresha huduma za upatikanaji wa afya katika kituo cha afya Endabash.
Mh. Kayanda ametembelea ujenzi wa miundo mbinu ya maji Kansay ambayo serikali imeshatoa Mil 125
za kusambaza maji DP 7 za jamii na kujionea maendeleo ya Mradi. Mradi huo wa maji utakakamilika mwishoni mwa mwezi wa nane tarehe 30 kwa mujibu wa mkataba. Mh. Kayanda ametemebelea DP ya Shule ya msingi Geer ambayo ina hudumia takribani familia 4414. Ameelekeza uongozi wa kijiji cha kambi ya Faru kukaa na kuandaa muhtasari utakaosaidia kamati ya maji ya kijiji hicho kuweza kupata nguvu ya kifedha kununua nishati ya umeme kwa ajili ya kusukuma kwenye matanki ya maji. Ameelekeza kamati ya maji kuhakikisha inarejesha fedha hizo za kijiji kwa wakati na kuhakikisha mradi huo unaweza kujiendesha wenyewe. Mh. Kayanda ameelekeza wajumbe wa kamati ya maji kutumia muda wa usiku kuvuta maji kwenye tanki ili wananchi waweze kupata huduma ya maji wakati wa mchana.
Mh. Abbas Kayanda akizungumza na wananchi katika Zahanati ya Ngaibara.
Mh. Kayanda amewatahadharisha uongozi wa kijiji kuepuka matumizi mabaya ya fedha au ubadhilifu wowote katika uendeshaji wa mradi wa maji. Amewaasa viongozi kulinda na kutunza miundo mbinu ya maji ili iweze kusaidia wananchi. Amesema kumekuwa na kasumba za matukio ya kuharibu miundo mbinu ya maji kwa kukata mabomba au kutoboa mabomba kwa misumari jambo ambalo linahatarisha huduma upatikanaji wa maji na kugaharimu katika kukarabati miundo mbinu ya maji. Amesema atakayebainika kuhujumu miundo mbinu ya maji atakamatwana kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa