• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Complains |
Karatu District Council
Karatu District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dhamira na Dira
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
    • Vitengo
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
  • Madiwani
  • Miradi
    • TASAF
    • BOOST
  • Machapisho
    • Hali ya Uwekezaji
      • Business License Form
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Habari
    • Hotuba kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha

UTENDAJI MZURI WA KAZI NI HESHIMA KWA UMMA

Posted on: July 9th, 2020

NA TEGEMEO KASTUS

Dhamana tuliyopewa kama watumishi ni kutumikia wananchi wanyonge, ambao wengi wanakuja kwenye ofisi zetu. Lakini wengine tunawafuata vijijni kwa ajili ya kwenda kuwahudumia, lazima tutoe kauli zenye dhamira ya kuwasaidia. Lazima watumishi tuwe mfano kwa kuheshimu mipaka ya kazi.

Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Abbasi Kayanda wakati akiwa anazungumza na wakuu wa idara  na vitengo wa Halmashauri ya Karatu. Mh. Kayanda amesema lazima watumishi walinde rasilimali za serikali, amesema rasilimali ni pamoja na afya ya mtumishi mwenyewe, lakini pia kutunza samani za serikali.

Mh. Kayanda amesisitiza kwa wakuu hao wa idara na vitengo juu ya kujenga mahusiano katika utendaji wa kazi. Jambo ambalo litasaidia watumishi kufanya kazi kama timu moja badala ya kufanya kazi kwa makundi.  Ameonya juu mahusiano yasiyokuwa na tija katika shughuli za serikali, amesema katika utekelezaji wa majukumu ya serikali undugu na urafiki unauwekwa pembeni.

Wakuu wa idara wa Halmashauri wakiwa wanasikiliza kwa makini Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Abbasi Kayanda katika kikao kwenye ukumbi wa Halmashauri Karatu

Mh. Kayanda amesema lazima kuwe na uwazi wa fedha zinazoletwa kwenye Halmashauri, lazima wakuu wa idara wafahamu ili waweze kusaidiana katika kutekeleza miradi ya maendeleo. Mh. Kayanda amesema bado kuna udhaifu katika kushirikiana, amesema mathalani swala la wanafunzi kurudi shuleni kuna maelekezo mahususi yaliyotolewa na wizara ya afya katika kukabiliana na janga la corona.  Amesema je  wakuu wa  idara wamefuatilia juu ya utekelezaji wa maelekezo hayo mahususi ya wizara ya afya ??  amesema lazima tuwe na taarifa za wanafunzi waliokuja shule, na wanafunzi ambao hawajahudhuria tangu shule kufunguliwa. Amesema lazima tujitahidi  sana kutekeleza majukumu yetu ndio maana serikali inasema tusikae ofisini.

Mh. Kayanda amesema kuna fedha za miradi ambazo serikali imezileta mwisho wa mwaka wa fedha, amesema fedha hizo zimeingia kwenye utekelezaji wa miundo ya afya na elimu. Hizo fedha zinapaswa kukamilisha  ujenzi wa miundo mbinu ya miradi hiyo ndani ya kipindi za miezi mitatu na miradi iendane na thamani ya fedha iliyotolewa. Mh. Kayanda amesema kuna kasumba fedha inatolewa halafu inakaa muda mrefu kwenye akaunti ya shule amesema aina hiyo ya urasimu hapana na  haiwezekani kwa sababu fedha imekuja kwa kazi ya utekelezaji wa miradi.

Mkuu wa wilaya ya Karatu akizungumza na wakuu wa idara

Mh . Kayanda ameweka mkazo kwenye swala la vitambulisho vya wajasiriamali amesema kuna vitambulisho 12500 ambavyo imepewa wilaya ya Karatu. Amesema mpaka kufikia tarehe 31 mwezi huu lazima tuwe tumeuza vitambulisho zaidi ya nusu tulivyopewa. Amesema kila mkuu wa idara ahakikishe anasimamia kata yake kwenye zoezi la kuuza vitambulisho vya wajasiriamali, amesema  Jumamosi ijayo atakutana  na wakuu wa idara wote wamueleze wameuza vitambulisho vingapi na wanampango gani madhubuti wa kuviuza vitambulisho vya wajasiriamali.

Mh. Kayanda amegusia juu ya hali ya usafi amesema mji wa Karatu ni mchafu, sheria za usafi zipo. Ametoa maelekezo kwa mkuu wa idara ya afya pamoja na Afisa mamlaka ya  mji mdogo kuja na mkakati wa kufanya mji uwe msafi. Amesema wananchi wapewe elimu kila mtu afanye usafi kwenye eneo lake. Amesema kuna kasumba ya watu kuchukua mifuko ya takataka na kuitupa kwenye mitaro ya barabara na watu kutitririsha maji machafu, amesema hilo haliwezekani. Karatu ni mji wa utalii lazima tubadili madhari ya mji wetu.

Mh. Kayanda amegusia juu ya migogoro mbalimbali amesema kuna migogoro iliyondani ya uwezo wa wakuu wa idara lazima iishe, amemuelekeza Afisa radhi kushughulikia mgogoro wa adhi juu ya mipaka wa kijiji cha Masabeda na Endala. Amesema hataki migogoro inayokaa muda mrefu kama umri wa mtu, amesema maelekezo yanayotolewa na viongozi wa kitaifa au baraza nyie watumishi ni wajibu wenu kutekeleza.

Matangazo

  • Matokeo ya upimaji wa Kitaifa kidoto cha pili January 07, 2024
  • Halmashauri ya Wilaya ya Karatu Uchaguzi wa Wanafunzi wa kidato cha kwanza, 2024 December 18, 2023
  • Matokeo ya Darasa la Nne January 07, 2024
  • NAFASI ZA KAZI 2024 April 21, 2024
  • Angalia Zote

Taarifa Mpya

  • MILIONI 400 ZATOLEWA KARATU, KUJENGA MABWENI NA MADARASA EYASI SEKONDARI

    January 30, 2025
  • WASIMAMIZI WAASWA KUSIMAMIA VIAPO VYAO KUELEKEA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024.

    November 23, 2024
  • JESHI LA AKIBA MKAWE WAZALENDO KWA TAIFA

    November 23, 2024
  • HALMASHAURI YAZINDUA KITABU CHA MPANGO MKAKATI WA UKUSANYAJI MAPATO.

    November 19, 2024
  • Angalia Zote

Video

DC KOLIMBA ATATUA KERO TARAFA YA EYASI KARATU
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fursa za Uwekezaji

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Wizara ya Fedha na Mipango
  • Jamvi la Habari
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karatu District Council

    Sanduku la Posta: P.O Box 190

    Simu: +255 272970648

    Simu ya Mkononi: 0754773947

    Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa