Na Tegemeo Kastus
Upatikanaji wa dawa katika kituo cha afya Karatu umezidi kuimarika, baada ya vifaaa tiba na madawa ya muhimu kuwepo. Manunuzi ya madawa yaliyofanyika yameleta matumaini kwa wananchi wanaoutumia kituo hicho kama hospitali ya wilaya.
Hayo yamebainika baada ya Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Abbas Kayanda alipotembelea kituo cha afya Karatu ili kujiridhisha juu ya utoaji wa huduma za afya. Mh. Kayanda amesema amesema utoaji wa huduma za afya nzuri ni kipaombele cha kwanza, hasa ukizingatia kazi kubwa anayofanya Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Magufuli katika kuimarisha huduma za afya nchini.
Amesema huduma za afya ikimarishwa vizuri katika kituo cha afya Karatu, itasaidia kuwahudumia wagonjwa wengi wanaotoka Karatu na maeneo ya jirani. Amemuelekeza daktari kiongozi wa kituo hicho kuendelea kufanyia kazi changamoto zinazojitokeza katika utoaji wa huduma katika kituo hicho.
Katika hatua nyingine Mh. Abbas Kayanda ametembelea zahanati ya Sumawe kujionea maendeleo ya ujenzi wa zahanati hiyo ambayo kwa sasa wananchi kwa kushirikiana na uongozi wa kata ya Ganako wameshajenga choo ambacho kipo katika hatua za mwisho kwa umaliziaji.
Mkuu wa wilaya yaKaratu (kulia) akizungumza na wananchi katika kituo cha afya Karatu
Katika hatua nyingine Bi Laura Bambo amepongeza serikali kwa hatua za ufuatiliaji zinazofanywa na viongozi. Amesema hii inasaidia kuondoa urasimu katika utoaji wa huduma za afya kwa wananchi. Bi. Bambo amesema utoaji wa huduma za afya unaimarika sana, na kumekuwa na uwazi mkubwa kati ya watoa huduma pamoja na wananchi wanaopata huduma katika vituo vya afya vya serikali.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa