Tegemeo Kastus
Udhaifu wa watumishi wa afya wa kutokuwa na rejista ya madawa yanayoingia na kutoka katika vituo vya afya imesababisha upotevu wa dawa za serikali. Hali hiyo imeongeza mwanya wa dawa za serikali kupotea au kuchelewa kuagizwa kwa sababu ya kukosa takwimu sahihi ya kiasi cha dawa zilizoisha na takwimu ya dawa zinazohitajika katika vituo vya huduma ya afya.
Hali hiyo imebainishwa na Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Abbas Kayanda alipofanya ziara katika zahanati ya Ayalabe na Tloma katika tarafa ya Karatu. Katika ziara hiyo Mh. Kayanda amefanya ukaguzi wa store za dawa katika zahanati hizo ili kujiridhisha kama dawa zilizopo zinaendana na mahitaji ya kituo. Mh. Kayanda amemuelekeza Mkaguzi wa ndani na Mganga mkuu wa wilaya kufanya ukaguzi wa vituo vyote vya afya ili kujua hali ya upatikanaji wa dawa na ubadhidhilifu wowote utakaoonekana, wahusika warejeshe na hatua za kinidhamu zichukuliwe dhidi yao. Utaratibu wa kukagua dawa katika vituo vya kutolea huduma ya afya utakuwa unafanyika sasa kila baada ya miezi mitatu ili kupata takwimu sahihi za dawa zinazoagizwa MSD na dawa zilizopo katika vituo vya afya.
Mh. Abbas Kayanda katika stoo ya dawa zahanati ya Ayalabe
Mh. Kayanda amekemea tabia za baadhi ya wahudumu wa afya wasio waaadilifu katika kituo cha afya Karatu za kuwaelekeza wagonjwa kununua dawa katika maduka ya watu binafsi. Amesema hatua za kinidhamu zitachukuliwa kwa mtumishi yeyote atakayebainika kumuelekeza mgonjwa kununua dawa kwenye maduka binafsi, vitendo hivyo vinaenda kinyume na sera ya serikali ya kuboresha huduma za afya na upatikanaji wa dawa katika vituo vyote vya afya ili wananchi waweze kupata mahitaji yote ya kitabibu katika vituo vya afya vya serikali. Lakini pia kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko wa bima ya afya iliyoboreshwa inayowezesha kituo cha afya kuwa na uwezo wa kununua madawa kwa kujitegemea kulingana na mahitaji.
Mh. Abbas Kayanda akizungumza na wananchi waliokuwa wakisubiria huduma za afya katika zahanati ya Ayalabe
Katika hatua nyingine Mh. Kayanda ameelekeza kuandaliwa kwa utaratibu maalumu wa kuwajulisha wakinamama wenye watoto wadogo kuja kwa pamoja kupata chanjo ya polio kwa watoto wao badala ya utaratibu wa kuwaacha kuhudhuria kliniki kwa uchache kwa ajili ya kupata chanjo ya polio. Amesema chupa moja chanjo inahitaji kutumika kwa watu 17 hivyo kufungua chupa kwa watu wachache ni kuharibu chanjo hizo.
Wakati huo huo Mh. Kayanda amemuelekeza mganga Mkuu wa wilaya kushughulikia swala la malipo ya walinzi katika zahanati ya Ayalabe na Tloma waliokuwa wanadai malikimbizo ya mishahara. Ikiwa nipamoja na kuandaa utaratibu wa kuwaweka kwenye bajeti ili kuondoa changamoto ya malimbikizo ya madeni inayojitokeza mara kwa mara katika zahanati hizo.
Mh. Kayanda ameelekeza utaratibu ufanyike ili nyumba za wafanyakazi wa afya katika zahanati ya Tloma ziweze kupata huduma ya umeme. Katika ziara hiyo Mh. Kayanda ametembelea zahanati ya Gyekrum Arusha kujionea hali ya utoaji wa huduma katika zahanati hiyo.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa