Na Tegemeo Kastus
Kazi zote zinazofanywa na watumishi wa umma ni utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi, kila mmoja awajibike mahali pa kazi. Kata ya Mbulumbulu mambo mengi yametekelezwa na bado yanaendelea kutekelezwa, tumefanya kazi za barabara kazi za afya na kazi za shule.
Hayo yamesemwa na Mh. Elias Simpa diwani wa kata ya Mbulumbu kwenye Mkutano wa mwisho wa robo ya mwisho wa kamati ya maendeleo ya kata ya Mbulumbu (ward development committee) ambao umefanyika katika kijiji cha Sloham. Amesema licha ya jitihada hizo bado kuna miradi ambayo haijamalizika mathalani mradi wa bararabara unaoendelea kujengwa; ameomba viongozi wa kata wasipambane na watu pindi dosari itakapotokea bali watumie busara ya kuwasiliana na mratibu wa mradi wa utengenezaji wa barabara ya Mbulumbulu.
Maeneo ambayo yamebaki na hayawezi kufikiwa na wakala wa barabara vijijini watawasiliana na wadau ili wakusanye mafuta ili Greda iendelee kufanya kazi ya tengenezaji wa barabara. Mh. Simpa amesema wataanzia shule saidizi ya Kituma kuja makao makuu ya kata, ameomba wadau kuendelea kuchangia mafuta ili maeneo yote korofi yakarabatiwe, ametoa rai kwa wananchi wa Mbulumbulu kuendelea kutunza miundo mbinu ya barabara, miundo mbinu ya shule na miundo mbinu ya afya.
Kwa upande wake Afisa tarafa wa tarafa ya Mbulumbulu Ndg. Saitoti Zelothe amesema Mvua kubwa za masika na ushoroba wa wanyama pori uliokatisha katika eneo la hifadhi ya barabara vimeathiri kwa kiasi kikubwa barabara za ndani ya kata ya kambi ya simba. Amesema uongozi wa serikali wa kata umefanya mawasiliano na NCCA pamoja na watu wa PAMS ili waweze kusaidia eneo liloharibika ambalo lipo katika eneo la hifadhi kiasi cha km 3-4, ili liweze kupitika vizuri.
wananchi wakifuatilia taarifa ya mkutano wa maendeleo ya kata Mbulumbulu
Ndg. Zelothe amesema wamepata mwitikio chanya kutoka kwa wadau na mpango uliopo ni kukarabati barabara hizo za ndani zilizoharibika ili ziweze kupitika kwa urahisi. Amesema utekelezaji huo utafanyika kwa kuwaomba wakala wa barabara vitendea kazi kutengeneza eneo hilo ambao mpaka sasa wako eneo la maradi wakifanya ukarabati wa barabara iliyotengewa na serikali kiasi cha million 308 kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya kijiji cha kambi ya simba Mpaka lositete.
Ndg. Zelothe amesema Tarafa ya Mbulumbulu imefaidika na awamu zote za REA ila kuna changamoto za upatikanaji wa umeme upande wa kijiji cha lositete. Mkandarasi anaangalia upande sahihi wa kuchukua umeme kati ya Upper kitete au upande wa chini wa wilaya ya Monduli. Amesema mkandarasi tayari ameshaanza kusambaza nguzo katika eneo hilo na matarajio ni kwamba ndani ya muda mfupi nyaya zitawekwa. Amesema kuna wananchi wametoa kiasi cha 27000 kwa ajili ya kuunganishiwa umeme na bado hawajaunganishiwa, Ndg. Zelothe amesema ameshawasiliana na meneja wa tanesco ndani ya wiki mbili tatizo litakuwa limeshatatuliwa.Ndg. Zelothe amesema kuna baadhi ya taasisi ambazo hazijaunganishiwa na umeme licha ya kwamba taasisi hizo zilishatolewa taarifa za awali, ameahidi kuendelea kufuatilia na kuweka msukumo ili taasisi hizo zipate umeme.
Ndug. Zelothe amesema serikali ya awamu ya tano chini Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli imeshatoa fedha kwa ajili kukamilisha miradi mbalimbali iliyokuwa imesahaulika kwa muda mrefu. Amesema kwa tarafa ya Mbulumbulu kulikuwa na mradi wa zahanati ya Kainam Rhotia, zahanati ya Kilimatembo na shule ya sekondari ya Upper kitete. Amesema yeye kama Afisa Tarafa jukumu lake kwa sasa ni kuhakikisha mradi unaendana na dhamani ya fedha iliyotolewa (value of money). Ndg. Zelothe amesema amejiwekea ratiba kila siku mchana lazima akague miradi miwili katika eneo lake la kazi ndio maana miradi mingi katika tarafa ya Mbulumbulu imeweza kukamilika ndani ya wakati.
Naye Afisa Mtendaji kata Ndg. Elikana Sulumbu amesema wakati akitoa taarifa ya utendaji kazi wa kata ya Mbulumbulu, wamepokea kero 531, kero zilizotatuliwa ni 529. Amesema katika kero hizo 529 kero za ndoa ni 18 kero za za fedha 126, kero za migogoro ya ardhi 119 na kero za kutelekeza watoto 63. Amesema watumishi na viongozi wa umma wamesaidia kutatua kero hizo kwa kiasi kikubwa, amesema hayo yamewezekana kutokana na kufanya kazi kwa kushirikiana. Amesema kasi ya watu kupeleka mashauri ya kesi mahakamani imepungua kwa kiasi cha 80% ameongeza kusema hata kiasi 20% walioenda mahakamani walishinda kesi zao.
wananchi katika matukio tofauti kwenye mkutano wa maendeleo kata ya Mbulumbulu
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa