NA TEGEMEO KASTUS
Kampuni ya carbon Tanzania imefanya makubaliano ya biashara ya hewa ya ukaa na vijiji na jamii ya Endesh, Dumechand, Jobaj, Mbuga Nyekundu, Qangdend, Mikocheni, na Endamaghan. Mkataba huo umeandaliwa chini ya sheria ya ardhi ya vijiji na 5 ya mwaka 1999 na sheria ya mikataba ya mwaka 2002.
Akizungumza baada ya uwekaji wa saini wa mkataba huo Meneja na muwekezaji wa kampuni ya Cabon Tanzania Ndg, David Beroff amesema wananchi wa vijiji husika toka zamani walikuwa wanahifadhi mazingira kwa manufaa yao na wamekuwa wanatoa faida kubwa kwa dunia kutokana na uhifadhi wa mazingira.
Picha katika matukio mbalimbali wakati wa uwekaji wa sahihi wa mkataba wa kibiashara ya hewa ya ukaa kati ya muwekezaji Kampuni ya Carbon Tanzania na viongozi wa kijiji Pamoja na jamii.
Amesema sasa ni wakati wa dunia kutambua na kuhamasisha juhudi za utunzaji wa mazingira ambazo kampuni ya Carbon Tanzania itakuwa na kazi ya kuingiza hewa ya ukaa kwenye soko la dunia. Wananchi wa vijiji husika watanufaika kwa sababu mazingira yataendelea kuwa mazuri zaidi kutokana na msukumo mkubwa watakaokuwa nao katika utunzaji wa mazingira. Amesema wananchi wa vijiji hivyo wataweze kupata faida ya kipato kupitia serikali za vijiji husika fedha ambazo zitasaidia serikali za vijiji hivyo kuwekeza katika shughuli nyingine za maendeleo.
Afisa mazingira wa wilaya Ndg. Ally Mdangaya amesema mradi huu unahamasisha wananchi watunze mazingira katika maeneo yao. Amesema kama vijiji vitakubaliana kufuata masharti ya mkataba misitu itatunzwa na itasaidia kuongeza pato la kijiji. Ameongeza kusema kwa uzoefu ambao wamepata kwa wilaya ya jirani ya Mbulu ambao mradi huo umeshaanza vijiji vya Tarafa ya Eyasi vitakuwa vimepiga hatua kubwa kimaendeleo.
Mwenyekiti wa kijiji cha Endesh Ndg. Geway Namagi akizungumzia juu ya uwekaji wa saini na kampuni ya Carbon Tanzania, amesema wanataraji kupata manufaa makubwa sana kutokana na kuwa na maeneo makubwa ya malisho na misitu hivyo uwekezaji huo utasaidia serikali za vijiji kuwekeza katika miradi ya maendeleo katika maeneo yao. Amesema kazi waliyonayo sasa ni kuhamasisha wananchi waongezee juhudi katika kuhifadhi mazingira.
Viongozi wa kijiji wakiwa katika picha ya pamoja na muwekezaji wa Kamapuni ya Carbon Tanzania
Muwekezaji huyo kampuni ya Carbon Tanzania ameingia mkataba wa miaka 20 ya uwekezaji wa hewa ya ukaa na viongozi vijiji hivyo katika ofisi ya Afisa tarafa wa Eyasi katika zoezi lilosimamiwa na Afisa Sheria wa Halmashauri ya wilaya ya Karatu.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa